Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 23, 2013

TID MNYAMA AISAMBAZA 'RAHA'


Na Elizabeth John

BAADA ya kutamba na kibao cha ‘Kiuno’ msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohamed ‘TID’ anatarajiwa kusambaza kibao chake kipya hivi karibuni kinachokwenda kwa jina la ‘Raha’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, TID alisema, kazi hiyo imekamilika na yupo katika hatu azamwisho za kutaka kuisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

“Nina imani itapokewa vema na mashabiki kutokana na ujumbe iliopo ndani yake ikiwa ni pamoja na mashairi ambayo yamesimama n akuburudisha jamii nzima bila kubagua rika,” alisema TID.

TID, aliwataka mashabiki na wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi hiyo, ambayo anaamini ataisambaza pamoja na video yake ili kuwapa raha mashabiki wa kazi wake.


Mbali na kazi hizo, msanii huyo alishawahi kutamba na vibao chake kama, ‘Asha’, ‘Nipe raha’ na nyinginezo ambazo zilimtambilisha katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...