Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 23, 2013

WANANCHI WA WILAYA YA BAGAMOYO MKOANI PWANI WATOA MAONI KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA.


Bmoyo1Mratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya Mohammed akiongea katika mkutano wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013). Wengine kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo Bw. Omar Sheha, Dkt. Salim Ahmed Salim na Alhaji Said El-Maamry.
Bmoyo2Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza Mratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya Mohammed  (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa majadiliano mjini humo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013).
Bmoyo3 Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mzee Omary Yahaya Mhando akitoa maoni yake katika mkutano wa Baraza hilo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013) mjini Bagamoyo. Bmoyo4Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Jumanne Chiboko akitoa maoni yake kuhusu rasimu ya katiba wakati wajumbe hao waliojigawa katika makundi. Mkutano huo umefanyika leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013) mjini Bagamoyo.
Bmoyo5Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Omar Sheha (kushoto) akiongea na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo (kulia) ambao wataongoza majadiliano ya makundi kabla ya kuanza kwa majadiliano kuhusu rasimu ya katiba. Mkutano huo umefanyika mjini Bagamoyo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2013) mjini Bagamoyo. (PICHA NA TUME YA KATIBA)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...