Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bw Sunil Colaso akiwashukuru watanzania kwa kutumia
huduma za Airtel wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea sokoni na
kupeleka kwa watanzania promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa.
Afisa
kitengo cha rasilimali watu Airtel Tanzania bi Josephine Kajembe
akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel money yatosha na promosheni
ya Airtel money Hakatwi mtu hapa wakati wafanyakazi wa Airtel
walipotembelea wateja sokoni katika maeneo mbalimbali jijini Dar es
saalam
Wafanyakazi
wa Airtel wakijipanga tayari kuingia sokoni na kuitambulisha promosheni
ya Airtel money Yatosha na kutoa elimu juu ya huduma zake hususani
Airtel money kwa watanzania jijini Dar es Saalam.
Mkurugenzi
wa mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya akiongea na watanzania juu
ya huduma ya Airtel money yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel
walipotembelea sokoni na kupeleka kwa watanzania promosheni ya Airtel
money Hakatwi mtu hapa.
...................................................................................................................................
Wananchi
katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam leo wamepokea kwa
kishindo promosheni ya Airtel money yatosha inayofahamika kwa jina la Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo
Promosheni
hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wa Airtel kutembelea
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaa na kutoa elimu juu ya huduma
mbalimbali na kuitambulisha rasmi sokoni promosheni ya Airtel money
yatosha hakatwi mtu hapa
Baadhi
ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema
kuwa huduma hiyo ya Airtel money Hakatwi mtu hapa imeweza kurahisisha
baadhi ya kazi zao na kuwawezesha kuhifadhi kiasi flani cha fedha
ambacho awali kilikuwa kinakatwa kutokana na kutuma na kutoa pesa.
“Katika
biashara zangu mimi huwa natuma na kupokea pesa mara nyingi tu, lakini
awali nilikuwa nakatwa kiasi flani cha pesa ambacho mtu mwingine anaweza
akaona kidogo lakini si kidogo ni kikubwa sana. Naishukuru Airtel kwa
huduma hii ya Hakatwi mtu maana inanisaidia kiuchumi pale ninapotuma na
kupokea pesa bure,” alisema Said Mrisho mfanyabiashara ndogondogo katika
soko la Tandika.
Akizungumza
na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil
Colaso alisema “ Airtel tunawajali wateja wetu na kwetu mteja ni namba
moja na ndio maana kwa mara nyingine tena wafanyakazi wote wa Airtel leo
wanaingia sokoni ili kutoa elimu na kuwaelimisha watanzania na wateja
wetu juu ya huduma zetu haswahaswa promosheni maalumu ya Hakatwi mtu
hapa .
Tunazo
huduma nyingine nyingi ambazo tunazitoa kwa wateja wetu kama vile Data
3.75G, Airtel Yatosha , na Huduma ya Airtel money ambayo sasa
tunaendelea kuiboresha zaidi na kuwapa wateja wetu fulsa ya kutuma na
kupokea pesa bure bila makato yoyote.
Lengo
letu ni kuhakikisha Airtel inaendelea kutoa huduma zilizo na ubunifu,
za kisasa zinazokithi mahitaji ya wateja wake na tunaamini Airtel money
hakatwi mtu ni suluhisho sahihi na litaleta unafuu katika huduma za
kifedha nchini
Akizungumza
katika ziara Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Bi Beatrice Singano
alisema” watu wameonesha muitikio mkubwa sana katika kuipokea huduma
yetu ya Airtel money hususani promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu na
hiyo inaonesha wazi ni jinsi gani Airtel inavyotoa huduma zilizo bora
na zinazokubalika kwa wateja wake na jamii nzima kiujumla.
“Promosheni
hii ya Hakatwi mtu hapa inawawezesha mtu kutuma na kupokea pesa bure,
yaani bila makato yoyote hivyo nachukua fulsa hii kuwahimiza watanzania
kutumia huduma zetu za Airtel money ambazo ni rahisi , salama na
zinapatikana nchi nzima
Ili
kutumia huduma ya Airtel money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na
kuunganishwa moja kwa moja na menu ya Airtel money kisha kufanya miamala
mbalilimbali ikiwemo kutuma pesa, kulipa bill, kuongeza salio kununua
LUKU, USA visa na nyingine nyingi. Aliongeza Singano.
Mwisho
No comments:
Post a Comment