Na Esther macha wa matukiodaima.com ,Mbeya
TAASISI za kifedha zimetakiwa kuwa rafiki wa mkulima kwa karibu katika
kuwapatia mikopo wakulima na kwamba mkulima anapofika kwenye taasisi
hizo kwa ajili kuomba kupatiwa mkopo hupata shida kupatiwa mkopo huo
tofauti na wafanyabiashara wakubwa.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu wakati
alipotembelea mabanda ya wakulima katika John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema kuwa baadhi ya taasisi za kifedha zimekuwa na
kasumba mbaya kwa wakulima ambapo zimekuwa zikiwabagua wakulima hao
pindi wanapofika kuomba msaada wa kukopeshwa.
Aidha
Bw. Mwambungu alisema kuwa wafanyakazi wa mabenki na taasisi zingine za
kifedha wanatakiwa kuwa karibu na wakulima hao pia watumie zaidi
taaluma na uzoefu wao wa namna ya kuwasiadia wakulima hao ili waweze
kujiinua kiuchumi.
Alisema
kuwa mabenki na taasisi za kifedha zinatakiwa kuondokana na kasumba
kwamba kwa vile ni mkulima hivyo hana uwezo wa kurejesha mkopo na
kuwathamini sana wafanyabiashara pekee wakati mkulima akipewa elimu juu
ya matumizi sahihi ya fedha anazokupeshwa anakuwa na uwezo mzuri tu wa
kurejesha mkopo huo.
“Mkulima
huyu apewe elimu na taasisi hizo juu ya ureshaji wa fedha hizo, hapo
atakuwa na urejeshaji mzuri katika fedha hizo”alisema Bw. mwambungu.
Alisema
kuwa Mkulima bila ya kusaidiwa kwa vitendea kazi ataendelea kupiga
hatua moja mbele na kurudi hatua tatu nyuma badala ya kusonga mbele na
kwamba hata maonyehso hayo ya wakulima hayata kuwa na maana kama
hawatapewa msaada wowote hususani taasifi za kifedha kuwapatia mawazo ya
kuwawezesha kupiga mbele zaidi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment