Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 24, 2013

LIGI ya Mpira wa pete (CHANETA CUP) inayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya imeanza kwa kasi baada ya timu nane kutoana jasho katika Mechi za ufunguzi.


 Timu ya Magereza kutoka Mkoani Morogoro iki ichachafya timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya maarufu kama Hamambe katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na ufundi wa wafungaji wa pande zote mbili



Mwenyekiti wa CHANETA mkoa wa Mbeya dadaMary akiongea na waandishi wa habari

Add caption


LIGI ya Mpira wa pete (CHANETA CUP) inayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya imeanza kwa kasi baada ya timu nane kutoana jasho katika Mechi za ufunguzi.
Mechi nne za ufunguzi zililazimika kufanyika Asubuhi kutokana na kufunguliwa kwa pazia la Ligi kuu la mpira wa Miguu kati ya timu ya Kagera Sugar na Mbeya City  katika uwanja huo huo hivyo kupisha muingiliano wa Ratiba.
Katika mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu za Polisi Mbeya iliyomenyana vikali na timu ya Tumbaku kutoka Mkoani Morogoro ambapo Timu ya Tumbaku iliibuka kidedea kwa magoli 35 dhidi ya 17 waliyoyapata timu ya Polisi Mbeya.
Mchezo uliofuata ulikuwa kati ya timu ya Jeshi la Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam dhidi ya Polisi Arusha na matokeo kuishia kwa Uhamiaji kuibuka na ushindi wa Magoli 27 kwa magoli 19 ya timu ya Polisi ya Arusha.
Timu za Polisi zilizidi kumwagiwa magoli katika Mchezo wa Tatu uliozikutanisha timu ya Polisi Mwanza dhidi ya Timu ya Filbert Bayi ya Dar Es Salaam ambapo timu ya Polisi ililala kwa magoli 21 dhidi ya magoli 33 ya Filbert Bayi.
Timu ya Magereza kutoka Mkoani Morogoro pia ilichachafya timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya maarufu kama Hamambe katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na ufundi wa wafungaji wa pande zote mbili ambapo hadi kipenga cha mwisho cha mchezo huo Hamambe magoli 28 na Magereza 31.

Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...