Kiungo wa zamani wa Yanga na Azam, Abdi Kassim
‘Babi’ amejiunga na mabingwa wa Zanzibar, Kikosi Maalum Kuzuia Magendo (KMKM).
Babi ambaye msimu uliopita aliichezea Azam lakini
aliachana na klabu hiyo baada ya kukataa kuongeza mkataba mwingine, aliambia
kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa amejiunga na timu hiyo jana bila kutaja
dau alilosajili wala urefu wa mkataba wake.
Kiungo huyo ambaye pia alicheza soka la kulipwa
nchini Vietnam aliandika katika uikurasa wake kuwashukuru viongozi wa KMKM kwa
kufanikiwa usajili wake na ana furaha kuitumikia timu hiyo katika msimu huu wa
Ligi Kuu ya Zanzibar.
Babi ambaye pia huitwa Barrack wa Unguja aliandika
maneno yafuatayo,
“hi nyote ...nashukuru Mungu mzima wa afya ...nimesaini
mkataba na KMKM, mabingwa wa soka Zanzibar na timu inayoshiriki mashindano ya
kimataifa na mashindano mbalimbali.
“...ikiongozwa na kocha mzoefu na mwenye ujuzi wa hali
ya juu, Ali Bushir ...so natoa shukrani za dhati kwa uongozi wa KMKM kwa
kumaliza zoezi la usajili kati yangu na wao na napenda kuwashukuru wapenzi wa KMKM
kwa kuniunga mkono.
“Nafurahi zaidi kwa vile nipo nyumbani na familia
yangu na biashara zangu za hapa na pale...asanten sana watanzania wote.”
No comments:
Post a Comment