Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 19, 2013

MBOWE AWATAKA WATANZANIA KUJADILI RASIMU YA KATIBA NA KUTOA MAONI VYEMA


IMG_2543
Helikopta maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma. Picha na Zainul Mzige 
IMG_2579
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

IMG_2610
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
IMG_2604
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara.
********************************************
Na. Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Chama cha Domekrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh.FREEMAN MBOWE amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya ili ipatikane Katiba itakayokidhi haja ya Watanzania.
Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani waMwanza alipokuwa kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa chama hicho kuunga mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwepo Serikali tatu siyo mzigo kama Chama cha Mapinduzi (ccm) kinavyosema ila tunataka kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na ile ya muungano ili kuleta usawa ndani ya Muungano huo.
Pia amesema kuwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili ipatiwe kipaumbele kufundishwa kuanzia daraja la awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea Watanzania kufahamu Lugha ya Kiingereza vema na kupata ajira kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...