Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 7, 2013

KONYAGI WAIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI KATIKA ZAO LA ZABIBU  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distileries Limited (TDL), David Mgwassa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu kuiomba serikali kuondoa kodi inayotoza kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado hakijajiimarisha kiuzalishaji. Kushoto ni Mwakilishi wa waandishi wa habari wa kiwanda hicho, Spear Patrick.
Mgwassa akijibu maswali kutoka kwa wanahabari
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distileries Limited (TDL), umeiomba serikali kuondoa kodi inayotoza kiwanda hicho kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado hakijajiimarisha kiuzarishaji.
Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam ambapo alielezea wasiwasi wa zao kuja kudorora iwapo kodi hiyo itaendelea kutozwa.
Alisema kutokana na uendeshaji wa kampuni kwa miaka sita tangu ifufue mashamba ya zabibu miaka saba iliyopita kwa kuagiza mbegu kutoka Afrika Kusini ni kipindi kifupi kuanza kukatwa kodi. “Kipindi cha miaka sita kuanza kukatwa kodi ni mapema mno kwani bado hatujasimama sawasawa tunaomba serikali kuangalia kwa makini jambo hilo ili kunusuru kilimo cha zao hilo na kuwakomboa wakulima” alisema Mgwassa.
Alisema TDL kwa mwaka huu imenunua lita milioni 1.720 za zabibu na kuwa lita milioni 1.1 ni kwa ajili ya kinywaji cha Valuer na 0.7 zilienda kwenye bidhaa nyingine. Mgwassa alisema kwa mwaka jana kampuni hiyo imetumia sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua zao hilo ambapo mwaka huu watatumia bilioni 2.3 na kuwa hali ya kilimo cha  zao hilo ni nzuri pamoja na soko lake tofauti ni inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Aliongeza kuwa iwapo serikali itaendelea kotoza kodi hiyo upo uwezekano wa vinywaji vinavyozarishwa na kiwanda hicho bei yake kuwa juu kutokana na bei ya soko kulingana na ile ya vinywaji kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...