Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 20, 2013

OPERESHENI YA KUONDOA WAHAMIAJI HARAMU SASA KUANZA GHAFLA KIMYA KIMYA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini  Dar es Salaam kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais Jakaya Kiwete   alilolitoa Juni 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa wa Kagera.
Kamishina Mkuu wa Uhamiaji Bw.Magnus Ulungi (kulia mbele) na Afisa Uhamiaji Mrakibu Bi.Rosemary Mkandala wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi  alipozungumza na waandishi wa habari leo jijini  Dar es Salaam kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais Jakaya Kiwete  alilolitoa Juni 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa wa Kagera. Picha na Lorietha Laurence –Maelezo
********************************************************
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu katika Kanda ya Ziwa itaanza kwa ghafla, huku  ikiendelea kusisitiza kwamba  watu wanoaishi nchini bila taratibu za kisheria kuondoka kwa hiari na mali zao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais Jakaya Kiwete   alilolitoa Juni 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa wa Kagera.

“Nimeshapewa maelekezo  rasmi na Rais Jakaya Kikwete ya kuwaondoa wahamiaji haramu nitakapoona inafaa. Operesheni itaanza ghafla haiko mbali. Muda mwuafaka wa kutekeleza vyombo vya dola vitasema.

“Tunatoa wito waondoke wenyewe na mali zao bila kunyang’nywa. Wenye mali nyingi wanatakiwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi ili waweze kusindikizwa. Hatutawavumilia wahamiaji haramu,” alisema Waziri Nchimbi.

 Aliongeza kuwa wahamiaji hao  wanaotaka kuishi nchini wanatakiwa kurudi nchini kwao kwanza na kufuata taratibu za kisheria kama ambavyo nchi nyingine zinavyofanya mtu akitaka kuishi nchi yoyote anatakiwa kufuata taratibu hizo.

Waziri alitoa onyo kwa viongozi wa vijiji wanaoshirikiana na wahamiaji hao kuwatunza na kusema jambo hilo ni makosa kisheria , hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

 Akizungumzia kuhusu takwimu za wahamiaji hao waliorejea nchini kwao mpaka sasa ni 10,672 kati ya  hao Wanyarwanda ni  6,088, Warundi 4000 na Waganda 269  ambao wametoka mkoa wa Kagera. Kwa wa mkoa wa Kigoma  ni  Warundi 142, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nane na katika mkoa wa Geita Wanyarwanda  126 na Warundi 39.

 Hata hivyo Waziri Nchimbi alisema  kuna wahamiaji  14 wamerejea nchini tena baada ya kurudi makwao na kuwataka wasilione jambo hilo kuwa ni mzaha.

 Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali ya Tanzania inashukuru ushirikiano unaotolewa na nchi wanazotoka wahamiaji hao kwa kuwapokea vizuri.

 Alifafanua kuwa suala la kuwarudisha wahamiaji  hao si la mara ya kwanza, lilishawahi kutokea. Huku akisisitiza kwamba tatizo linatokana na sababu mipaka yetu mikubwa na kuna watu wasio  wazalendo  ambao wanawapokea na kuwakaribisha kwa kupatiwa zawadi. Hivyo Serikali inalifanyia kazi jambo hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...