Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 16, 2013

ZIARA YA KUSHITUKIZA YA DKT MWAKYEMBE UWANJA WA NDEGE YAZAA MATUNDA, ANASWA MMOJA NA MADAWA


Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana  Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine.Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akionyesha picha ya kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya ghafla kweny Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Picture 234Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza  Dkt. Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe. 
***************************

JITIHADA za Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo…,” alisema.
“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...