Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 13, 2013

ABDUKIBA AWASHTUKIZA MASHABIKINa Elizabeth John


BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Kidela’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdukarim Kiba ‘Abdukiba’ anajipanga kuwapa ‘Surprise’ wapenzi wa kazi zake hivi karibuni.

Mbali na Kidela, Mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Kizunguzungu’ na ‘Huyo sio demu’ ambazo zilimtambulisha n akufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es salaam, Abdukiba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambacho hakutaka kukitaja jina ili asiwatayarishe wapenzi wa kazi zake.

“Unajua nikitaja jina wataanza kutafakari ni nini nimezungumzia ndani yake nataka kuwashtukiza ila ninachowaomba wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo,” alisrma Abdukiba.


Alisema kazi hiyo anatarajia kuanza kuisambaza baada ya wiki mbili na itakuwa ni pamoja na video yake ambayo ameitengeneza sehemu mbalimbali za jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...