Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 30, 2013

ETO`O NA MOURINHO WAUNGANA TENA CHELSEA BAADA YA MCAMEROON HUYO KUANGUKA MKATABA WA MWAKA MMOJA


Parading: Eto'o has signed for ChelseaJembe la nguvu: Eto’o amesaini Chelsea leo  Pen to paper: Eto'o signs the contract in the presence of Chelsea club secretary and director David BarnardKalamu kwenye karatasi: Eto’o amesaini mkataba mbele ya katibu na mkurugenzi wa Chelsea  David Barnard 
Pleased to be here: Eto'o has signed on a free transferNimefurahi kuwepo hapa: Eto’o amesaini kwa uhamisho wa bure na amesema amefurahi kuwepo darajani
 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KLABU ya Chelsea imethibitisha kumsajili bure mshambuliaji raia wa Cameroon, Samuel Eto’o .
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32- inafahamika kuwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa dau la  pauni milioni 7 , japokuwa atapunguziwa mshahara wake kwani mpaka sasa ndiye alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani, dau la pauni milioni 17 kwa mwaka katika klabu ya  Anzhi Makhachkala.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho  amekata tamaa kumshawishi mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Mark Rooney baada ya ofa zake kutupiliwa mbali na David Moyes, na sasa amegeukia mpango B ambapo amelinasa jembe hilo la Kiafrika.
Mourinho na  Eto’o wamekutana tena kwani walishawahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Inter Milan na kutwaa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...