Ngorngoro Heroes kuzindua Uwanja wa Aman
Na Addolph Bruno
TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', imealikwa kwenda Zanzibar kushiriki kwenye sherehe za uzinduzi wa Uwanja wa Aman utakaofanyika Jumamosi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF Florian Kaijage alisema ikiwa Zanzibar, Ngorongoro Heroes itacheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu nyingine zitakazoalikwa.
"Leo kwa mara nyingine tena timu yetu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, imealikwa kwenda kushiriki sherehe za uzinduzi wa Uwanja wa Aman na hii ni fursa ya pekee kwa timu hiyo katika kuendeleza vipaji, Alisema Kaijage.
Alisema timu hiyo itacheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar 'Karume Boys' na baadaye itacheza michezo mingine itakayopangiwa.
Ofisa huyo alisema baada ya kupata taarifa hizo, timu hiyo imeanza kujiandaa ikiwa chini ya Mocha Mkuu wake, Rodrigo Strokler akisaidiana na Adolf Rishard.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa chini ya miaka 19 Copa Coca Cola wakiwa na mizigo yao kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara baada ya kuwasili jana wakitokea Afrika ya kusini walikoshiriki michuano ya Vijana wa Copa coca cola.
No comments:
Post a Comment