Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 4, 2011

EWURA Yapunguza Bei ya Mafuta


Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Haruna Masebu
Benjamin Sawe, Maelezo Dodoma

Serikali imepuguza bei ya mafuta ili kuwapunguzia makali watumiaji wa badhaa hiyo nchini.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa EWURA Haruna Masebu amesema mafuta ya petroli yamepungua kwa sh 202.37 sawa na asilimia 9.17 ambapo mafuta ya dizeli yatakuwa yamepugua kwa shilingi 173 ambay ni sawa na asilimia 8.32.

Bwana Masebu alisema alisema bei ya mafuta ya taa imeshuka kwa shilingi 181.37 sawa na asilimia 8.70 na mabadiliko hayo yametokana na marekebisho ya yaliyofanywa na kanuni kukokotolea bei za mafuta.

Alisema bei zingeshuka kwa sababu ya kupanda kwa bei katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa tahamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani.


Aidha Bwna Masebu alisema kwa mujibu ya Sheria ya mafuta ya mwaka 2008 bei za mafuta ya petrol I zitaendelea kupangwa na soko na EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petrol kwa bei ya ushindani pasipo kuongeza bei iliyopangwa na taasisi ya EWURA.

Pia vituo vya mafuta vimetakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili kuonyesha bei ya mafuta.

Kwa mujibu wa Bwana Masebu bei hiyo ya mafuta itaanza rasmi kutumika rasmi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...