Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 4, 2011

Zantel yadhamini Mkutano wa Kimataifa wa Masuala ya TEKNOHAMA


Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, William Mpinga (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu udhamini wa kampuni yake katika Mkutano mkubwa wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) ulioandaliwa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) utakaofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Kesho Jumatano. Zaidi wa ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo. Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Godwin Mjema na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kompyuta wa IFM, Jim Yonazi.

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Godwin Mjema (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, William Mpinga na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kompyuta wa IFM, Jim Yonazi.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Jim Yonazi (kulia), naye akielezea baadhi ya masuala mbalimbali yatakayojiri hapo kesho katika mkutano huo.
http://johnbadi.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...