Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 16, 2012

MABONDIA WA TAIFA WAWAGALAGAZA WAKENYA



MABONDIA wa timu ya Taifa ya masumbwi nchini imewagalagaza mabondia wa Kenya wakati wa
Mashindano ya Kimataifa ya Ngumi ya kirafiki yaliyofanyika leo katika  uwanja wa ndani wa taifa ambapo mashindano hayo mbali na kutokuwa na mzamini yalikuwa na msisimko wa ali ya juu kutokana na mwamko wa mashabiki wa mchezo uho uliokuwa ukifanyika katika uwanja huo

Katika mpambano uho bondia wa Kenya Matayo Keya alimtwanga kwa point bondia kutoka Tanzania Said Hofu na bondia Frank Mnene alimtwanga John Christian wa TZ nae Bondia wa Tz  George Constantno alimtwanga Isack Meja

Na bondia wa kike kutoka Tanzania Sara Andrew alipigwa na bondia wa kike kutoka kenya Gronna Kusa katika atua nyingine bondia Denis Martin wa Tanzania alimtwanga  Kamau Ng'ang'a wa kenya na bondia Mohamed Chibumbuli alimtwanga Edwin Okongo wa Kenya

Katika hatua nyingine Viongozi wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Masumbwi Nchini Kenya wamefurai kuwepo hapa kwa ajili ya kujipima nguvu kwa kuwa ni jumuiya moja ya Afrika Mashariki ambapo mashindano haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara kipindi cha nyuma ambapo mabondia wengi walikuwa wanakwenda kenya na wengine kuja nchini kwa ajili ya kupima viwango vyao

Nawo viongozi wa Chama cha mchezo wa Ngumi za Ridhaa BFT Mwenyekiti Michael Changalawe amesema mabondia wa Kenya wamejigalamia wenyewe kutokana na kutokuwepo na wazamini ambapo wengi wao wameupa kisogo kuzamini mchezo wa Masumbwi nchini unaopendwa na mashabiki wengi  hivyo amewataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia mchezo huu wa masumbwi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...