NA
MWANDISHI WETU ALIYEKUWA KISARAWE
BAADHI
ya watoto nchini wameitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Inayoongozwa na Jaji
mstaafu Joseph Warioba, kuweka kipengere katika Katiba Mpya
kitakachowalazimisha wawekezaji kununua magari kwa ajili ya wanafunzi.
watoto yaliyofanywa na utawala wakibaguzi Katika Kitongiji cha
Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976 wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari Makurunge walisema sheria hiyo inawezekana iwapo
viongozi watakuwa na dhamira ya kweli.
Walisema
kwa kuwa katiba ndio muongozo wa kila nchi hivyo wanaamini kuwa kipengere hicho
kitakapoingizwa kitawaongoza wawekezaji wenye nia ya kweli ya kuwekeza nchini
kufuata sheria hiyo.
Mmoja
wa wanafunzi hao, Sharifa Haroun ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika
shule hiyo alisema sheria hiyo inawezekana kwani zipo baadhi ya nchi kama
Botswana inacho kipengere hicho katika Katiba yake.
Alisema
kutokana na sheria hiyo nchini humo, wanafunzi wake wamekuwa wakienda shuleni kwa
kutumia magari yaliyonunuliwa na wawekezaji bila usumbufu.
Naye
Mwantumu Nassoro alisema sheria hiyo, itaangalia uwezo wa kila mwekezaji kisha
kupangiwa kiwango chake cha ununuaji wa magari hayo ya wanafunzi kwa mfano
kuana atakayeweza kununua 100, 200, 300 na wengine zaidi.
“Unajua
hivi vitu vinawezekana ikiwa viongozi wa nchi hii wataamua na tunatoa tahadhari
kuwa haya ni maoni karibu ya wanafunzi wote hivyo tunawaomba wasimamizi wa Tume
wayachukuwe na wayafanyie kazi”alisema Mwantumu.
Mwanafunzi
mwingine, Mwajuma Idrissa yeye alisema umefika wakati kwa viongozi na wadau
wengine kukumbuka zaidi maslahi yao zinapotokea fursa kama hizi zinazo nchi kwa
ujumla.
Alisema
wanataka mchakato unaoendelea wa upatikanaji katiba mpya lazima utowe nafasi
kwa watoto kuchangia kile wanachoona kitawasidia katika kuwaondolea kero zinazo
kwamisha jitihada zao za kujipatia elimu bora.
Aidha,
Mwajuma aliongeza kuwa, katika hilo la wawekezaji kununua magari ya wanafunzi
ni kwamba gari hizo itawalazimu kuzisimamia katika matengezo kila
yanapohitajika ambapo serikali itahusika katika kuyapangia maeneo ya kufanya
kazi hiyo nchini. Kwa habari zaidihttp://www.fullshangweblog.com/
Usually I don't read post on blogs, but I wish to say that this write-up very pressured me to take a look at and do it! Your writing taste has been amazed me. Thanks, very nice article.
ReplyDeleteHere is my site cellulite treatment reviews