Meneja wa masoko mkoa wa Iringa bw Philip Gucha kulia na mwakilishi wa kampuni
ya bia ya Serengeti Bw Shomari kushoto wakimkabidhi Bw. Fadhili Manzi zawadi ya
Bajaj mpya aliojishindia katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA
KIZIBO NA SBL HUKO MAFINGA MKOANI IRINGA JANA.
Kampuni ya bia ya Serengeti jana imekabidhi zawadi ya bajaji mpya na pikipiki mpya kabisa kwa washindi wa zawadi hizo mkoani
Iringa ambapo Bajaji ilikabidhiwa kwa Bw Fadhili Manzi katika mji mdogo
wa Mafinga mkoa humo na pikipiki ilikabidhiwa kwa Bw Fadhili Manzi
mjini Mafinga mkoa wa Iringa ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA
CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16 za
promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni
washindi wawili walipatikana ambao ni bw. Deusdedit Tobias Njau 22
kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya
na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye
amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake
siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano
hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa
na umati mkubwa wa watu
ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na
kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo
ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa
nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati
wa kukabidhi zawadi hizo meneja wa masoko SBL mkoa wa Iringa Bw. Philip
Gucha amesema washindi hao walipatikana
kihalali na kwamba kila mtanzania mwenye sifa zilizoainishwa katika
vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na
kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika
promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini zawadi hizi ni
robot u ya zawadi zite ambazo tunawasubiri ninyi watanzania na wateja
wetu wote kujishindia” alisemaGucha
na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya
Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya mtu haiwezi kwenda kwa
mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita
mfululizo ambapo bado takriban wiki 11 sasa ili kuisha kwa promosheni
hiyo ya pekee na ya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni
780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini
Kwa upande wake mshindi wa bajaj bw. Fadhili Manzi
amesema kwasasa safari ya maisha yake na familia yake itabadilika
kutokana na zawadi hiyo kwa ni sawa na mkulima hodari kuzawadiwa trekta
“Sasa wale vijana wenye uwezo wa kuendesha bajaj walete vyeti na leseni
zao za udereva wa bajaj ili niwape kazi kwani hii bajaj inaanza biashara
haraka iwezekanavyo” alisema Manzi ambaye alionekana kujawa na furaha
ya pekee na kutumia fursa hiyo kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti
kwa kumwezesha kupiga hatua kubwa kimaisha.
|
No comments:
Post a Comment