Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 10, 2012

TAIFA STARS YAICHAPA GAMBIA 2-1 UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', John Boko (kushoto) akimtoka beki wa timu ya Taifa ya Gambia, wakati wa mchezo uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Stars wameibuka kidedea kwa kuwachapa Gambia mabao 2-1. 
Gambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lililofungwa na mshambuliaji wake, MomodouCeesay, katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza, huku mabao ya Stars, yakiwekwa kimiani na beki wake, Shamari Kapombe, katika dakika ya 60 na bao la pili likifungwa kwa mkwaju wa penati na Erasto Nyoni, katika dakika ya 84, baada ya mshambuliaji wa stars, Mbwana Samatta, kumlamba chenga ya maudhi beni wa Gambia na kuunawa mpira huo.


Kwa matokeo hayo sasa, Stars imefikisha jumla ya pointi 3 katika kundi C na kupaa hadi nafasi ya pili nyuma ya vinara wa kundi hilo, Ivory Coast, ambao wanaongoza kundi hilo wakiwa na Pointi 4,  baada ya mchezo wake wa jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Morocco.

 Sehemu ya mashabiki wakiwa wamepoa jukwaani wakati Stars ilipokuwa nyuma kwa bao 1-0.
 Hata Rais wa kigeni walifika uwanjani kuishangilia Stars.
 Huyu naye pamoja na kuona kwa macho 'Live' mchezo huo lakini bado alikuwa na redio yake Booonge la Mkulima, akisikiliza matangazo ya mchezo huo uwanjani hapo.
Mashabiki wa Soka wa Stars, wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati.

 Mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars Mrisho Ngasa akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Gambia The Scorpions wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil, mchezo huo unafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hivi sasa mpira umekwisha Taifa Stars ikiifunga  Gambia magoli 2-1  na kujipatia pointi zake tatu za mwanzo, Magoli yamefungwa na wachezaji  Shomari Kapombe na Erasto Nyoni aliyefunga kwa njia ya penati baada ya mabeki wa timu ya Gambia kuunawa mpira katika eneo la hatari.
 Madaktari wakimtibu Mrisho Ngasa mara baada ya kuumia katika mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Gambia kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja.

1 comment:

  1. Nyc blog...but kuwa makini na maandishi cheki badala ya Raia wa kigeni unaandika Rais,Beki unaandika Beni

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...