Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 20, 2015

BONDIA WA MOROGORO AOMBA PAMBANO LA NGUMI KWA MAPROMOTA


Na Mwandishi Wetu 

PIUS KAZAULA
BONDIA Pius Kazaula wa Morogoro KG 66 amejitokeza hadharani na kuwaomba wadau wa mchezo wa masumbwi pamoja na mapromota kumwandalia mpambano kwa ajili ya kupima kiwango chake kwa kuwa mapromota wengi wapo Dar es salaam wao wa mikoani wanasahaulika

akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao mana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia wengine tupo mokoani tunafanya mazoezi tu bili kujipima viwango vyetu

hivyo napenda kutoa wito kwa mapromota kujitokeza kutusapoti sisi mabondia wa mkoani ili nasi tujipime na mabondia mnao waamini

najiamini kuwa naweza kazi hivyo nami wasinikwepe kwa kuwa nawataka mabondia wao nasikia Bagamoyo Mkoa wa Pwani nao wanandaa ngumi mara kwa mara wajaribu kutuita na sisi si Dar peke yake mabondia wapo nchi nzima hivyo mapromota kama wana nia kweli ya kukuza mchezo na kuendeleza ngumi chini wawe wanachanganya mikoa mbalimbali 

bondia huyo mwenye makazi yake Morogoro akusita kumpongeza kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sapoti anayotoa kwa mabondia mbalimbali na kuwapatia vifaa vya masumbwi  kwa galama nafuu na DVD zenye mbinu mbalimbali za mafunzo ya ngumi anazotoa kuelekeza mabondia chipkiz ambao wana kiu ya kuwa mabingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...