Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 1, 2015

NGUMI KUFANYIKA TENA BAGAMOYO JUNE 14 UKUMBI WA TASUBA


Na Mwandishi Wetu

NGUMI kupigwa tena Bagamoyo mpambano mkali wa masumbwi utakao wakutanisha Mfaume Mfaume wa Manzese pamoja na Adam Ngange wa Chanika utafanyika Bagamoyo katika ukumbi wa TASUBA siku ya june 14 ambapo watasindikizwa na mipambano mingine mikali siku hiyo

bondia Iddi Pialali 'Simba Aliyejeluiwa' atapambana na Sweet Kalulu wakati Raymond Mbwago atapambana na Haridi Hongo na Ramadhani Sebe atakabiliana na Said Kassim mpambano mwingine utakuwa ni kati ya bondia Abdalla Pazi' Mfalme wa wazalamu' atakae pambana na Haridi Van Dame' wa Kawe

siku hiyo pia kutakuwa na burudani za mziki wa kizazi kipya ambapo msanii Jumanne Iddi na Sam wa ukweli ambao watapamba burudani za mchezo uho wa masumbwi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...