Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 30, 2013

AFANYAKAZI WA MASHIRIKA YA UMMA WACHUANA KATIKA MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI YA SHIMIWI MJINI DODOMA


 Mkimbiaji wa mbio za Baiskeli wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Rajab Salum Sheikh (kushoto) akichuana na mpinzani wake wakati wa mashindano hayo ya Shimiwi, yaliyofanyika mjini Dodoma leo asubuhi, ambapo wakimbiaji walikimbia jumla ya Kilometa 36. Rajabu alimaliza mbio hizo na kushika nafasi ya tisa kati ya washiriki 22.
 Mkimbiaji wa mbio za Baiskeli wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Rajab Salum Sheikh (kushoto) akichuana na mpinzani wake wakati wa mashindano hayo ya Shimiwi, yaliyofanyika mjini Dodoma leo asubuhi, ambapo wakimbiaji walikimbia jumla ya Kilometa 36. Rajabu alimaliza mbio hizo na kushika nafasi ya tisa kati ya washiriki 22.
 Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliojitokeza kushuhudia mbio hizo.
 Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio hizo.
 Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio hizo.
Rajab, akipongezwa na wafanyakazi wenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais, baada ya kumaliza mbio hizo za Kilometa 36.

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LIKIENDELEA USIKU HUU NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.



Muigizaji wa filamu lakini pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,aitwaye kwa jina la kisanii Shilole akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa ccm kirumba usiku huu.
Anaitwa Christian Bella ambaye alikuwa akifanya vyema sana kwenye bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
Anaitwa Neylee,msanii wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema sana kwenye anga ya muziki huo,akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea 2013.
Pichani kati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel akiwa na marafiki zake wakilifuatilia tamasha la serengeti fiesta 2013 usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba,ambapo wakazi wa jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi.
Kila kona ni ileee full maraha tuu,huku wakiburudika na vunywaji mbalimbali kutoka kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la serengeti fiesta wakishirikiana na PSI kupitia bidhaa yao ya Salama kondom.
Vijana machachari kabisa kutoka kinondoni wakitambulika kwa jina la KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za Michael Jackson mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza.
Mmoja wa sanii waliofanya vyema sana katika shindano la BSS,Walter Chilambo,akiimba usiku huu kwenye jukwaa la Serengeti fiesta.
Mashabiki wa fiesta kibao usiku huu ndani ya ccm kirumba.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

BONDIA ZUMBA KUKWE AMGALAGAZA HAMADUU MWALIMU NYUMBANI KWAKE


Bondia Zumba Kukwe kushoto akimtupia ngumi Hamaduu Mwalimu wakati wa mchezo wao uliofanyika  kwenye ukumbi wa Temeke Mikoroshini ambapo ni nyumbani kwa hamaduu Kukwe alishina kwa K,o ya raundi ya tatu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii Sako Mtlya katikati akimwesabia bonia Hamadu Mwalimu baada ya kupokea konde zito kutoka kwa Zumba Kukwe kulia Kukwe alishina mchezo huo ka K,O ya raundi ya tatu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe akisagilia ushindi na Kocha wa Mkoa wa Pwani Agostin Uyaga baada ya kwisha mpambano huo
Bondia Mbena Rajabu Kushoto na Kassim Rajabu wakipambana wakati wa mpambano wao wa utangulizi
Matokeo ni Droo
Bondia Saidi Mwalimu kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Zakaria Kibwana wakati wa mchezo wao uliofanyika  katika ukumbi wea super sterio mwalimu alishinda kwa ko, ya raundi ya nne

MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO LA NEBRASKA NCHINI MAREKANI.


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea hati ya uraia wa hiari wa Jimbo la Nebraska nchini Marekani iliyotolewa na Secretary of State wa Jimbo hilo Bwana John Gale. Anayekabidhi hati hiyo kwa Mama Salma ni Dkt. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human sciences wa Chuo Kikuu cha Nebraska nchini Marekani
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akitoa keynote address kwenye' workshop on Viewing English Education through a Globalized Lens' iliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska huko nchini Marekani.
 washiriki.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Dr. Dzingai Mutumbuka, Chairman of the Association for the Development of Education in Afrika and Former Minister of Education in Zimbabwe mara baada ya Mama Salma kuhutubia mkutano Global Education huko Nebraska nchini Marekani tarehe 28.9.2013. Picha na John Lukuwi

Simba yaua Ruvu JKT 2-0

A; YAICHAPA JKT RUVU 2-0
 Wachezaji wa Simba na Ruvu JKT wakisalimiana kabla ya pambano lao la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
 Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimiliki mpira huku akizongwana na wachezaji wa JKT Ruvu, Nashon Naftali (kulia) na Emmanuel Pius wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa.

Friday, September 27, 2013

BONGO MOVIE KUIMBA SIYO LELE MAMA



STEVE NYERERE  pichani  naye kaachia ngoma japo anasema kwamba yeye anaimba kwa hobbie na siyo kusaka mahela.
Huenda, kutokana na mafanikio ya aliyekuwa msanii wa filamu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, labda ndiko kumewapa mshawasha wengine kujaribu kuimba kwa lengo la kupata mafanikio.

.............

WASANII wengi hapa nchini, hususan wale wa filamu ‘Bongo Movie’ wengi wao wameibuka na kutangaza kuacha kucheza filamu na kugeukia muziki wa Bongo Fleva.

Hii ni sawa, lakini je ni kweli wana vipaji vya kuimba ama ni kutaka kuuza sura tu?

Ni jambo la kawaida na zuri, kwa kila binadamu kuamua kuiga mambo mbalimbali yaliyo mazuri, ikiwa ni njia moja katika kusaka maendeleo binafsi.

Lakini katika hili, wasanii wa bongo movie, wengi wenu kugeukia muziki hiyo si sawa, kwani inaonesha dhahiri kwamba, wengi wao wanafuata mkumbo.

Kwa kufuata mkumbo huku, sina shaka kwamba, hata nyimbo watakazoziachia hazitakuwa na mashiko kama jinsi ilivyo kwa wasanii ambao tangu awali waliamua kujikita katika muziki.

Ushauri wa safu hii ni kuwaomba wajidhatiti katika kuandaa filamu zao, ambazo kwa ukweli usiopingika, nyingi zimekuwa zina upungufu mwingi ambao unahitaji marekebisho.

Lakini, badala ya kufanya masahihisho katika filamu zao na kuondoa makandokando yaliyomo, sasa  wanageuza mwelekeo na kukimbilia muziki, ambako nako sitarajii kama watatenda miujiza.

Nadhani, laiti kama wakiamua kujikita ipasavyo katika filamu na kutuliza vichwa vyao, sambamba na kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu fani hiyo, huenda wangefika mbali zaidi ya hapa walipo kwa sasa.

Inasikitisha kuona kwamba, msanii ambaye alikuwa anafanya vema katika filamu, kisha akageukia bongo fleva lakini anashindwa kufanya vizuri katika kuimba, hii itaweza kumshusha hata katika mauzo ya filamu zake bila ya yeye kujua.

Usanii ni pamoja na kukopi, lakini kwa kukopi kipaji cha mtu hii si sawa, kwani kila mtu amezaliwa na kipaji na uwezo wake, hivyo kwa kulazimisha kipaji ambacho siyo cha kwako, sidhani kama yupo ambaye atafanikiwa.

Huenda, kutokana na mafanikio ya aliyekuwa msanii wa filamu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, labda ndiko kumewapa mshawasha wengine kujaribu kuimba kwa lengo la kupata mafanikio.

Kwa upande wa Shilole, Mungu alimuumba na kumpa vipaji, kwani yeye alipotangaza kuwa muimbaji wa Bongo Fleva, alitoka na Aboubakar Katwila ‘Q- Chillah’ na wimbo wa ‘Sitaki Lawama’ akaonekana kama kabebwa, lakini  kwa kuwa ule ulikuwa ndiyo mwanzo, wengi wakasema acha tumpe nafasi.

Akaja akaachia ngoma nyingine ‘Paka wa Baa’, hapo kila mtu akamkubali na sasa anatamba na kibao cha ‘Nakomaa na Jiji’.

Hivi sasa, Shilole ameweza kupata mialiko mingi na kufanya maonesho kwenye matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Jina la Shilole, limekuwa kubwa na kazi yake inatambulika hata kama wapo ambao watasema amebebwa, lakini ukweli ni kwamba, uwezo wake unaonekana dhahiri.

Cha kushangaza kwa sasa ni hawa wasanii wengine wa filamu, kupanga mstari na kutangaza nia ya kuingia katika bongo fleva.

Sawa, tangazeni nia siyo vibaya, ila je mtaweza kumudu au mnadhani kuna mteremko huko?

Muziki siyo lele mama, lazima uwe na uhalisia na siyo mchezo wa maigizo kama jinsi mlivyozoea huku wakati mwingine ‘mkikopi’ kazi za watu na kuziweka sokoni.

Safu ya Busati, inawatahadharisha bila kificho, ingieni katika muziki lakini mje mkiwa kamili.

Baadhi ya wasanii ambao wametangaza kuimba ni pamoja na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Aunt Ezekiel, Rashida Wanjara, Mzee Magari, Rose Ndauka na wengineo wengi, lakini hadi sasa hakuna kipaji chochote kimeonekana na kufanya vizuri.

KATIBU MKUU WA OMR, SAAZ SALULA AITEMBELEA TIMU YAKE KAMBINI MKOANI DODOMA


 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati walipokuwa katika mazoezi yao leo asubuhi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI. Katibu Mkuu alipita kuwajulia hali wachezaji wake na kujua maendeleo ya kambi hiyo.
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akizungumza na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowatembelea kuwajulia hali katika Kambi yao mjini Dodoma leo wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI.
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ofisi yake, wakati alipofika katika Kambi ya timu hiyo kuwajulia hali mjini Dodoma leo asubuhi, wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ofisi yake, wakati alipofika katika Kambi ya timu hiyo kuwajulia hali mjini Dodoma leo asubuhi, wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI.

UJENZI WA VITUO VYA MABASI YAENDAYO KWA KASI WAENDELEA KWA KASI JIJINI DAR ES SALAAM


Mafundi wa kampuni ya Strabag ambao ni wajenzi wa barabara za mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi wakiendelea na ujenzi katika kituo cha Kimara kama ambavyo inaonekana katika picha

FILAMU MPYA ZA KAMPUNI YA STEPS AMBAZO ZIPO SOKONI

 







MAONYESHO YA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI YALIYODHAMINIWA NA NMB YAFANA


photo1
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga 26-27/9/2013. Walioambatana naye ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Nagu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Mh. Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Mkutano wa Uwekezaji Nd. Salum Shamte pamoja na viongozi na washiriki wengine. photo2Naibu Waziri TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho hayo. Kutoka kulia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo, Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa pamoja na wafanyakazi wa NMB Tawi la Madaraka Tanga. photo3 
Mkurugenzi Ukaguzi wa ndani wa Makampuni ya Impala Bw. Julius Makara (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Wateja Wakubwa Bw. Nsolo Mlozi baada ya kutembelea banda la NMB photo4Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo (kulia)akibadilishana mawazo na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB. Kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Pangani Farms Bw. Charles Makoi.
photo5 Mkurugenzi Mtendaji wa Pride (T) Limited Bw. James Obama (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo. Pembeni yake ni Meneja wa Tawi la NMB Madaraka Tanga Bw. Juma Mpimbi, Meneja Uwekezaji wa NSSF Bw. Abdallah Mseli na Meneja Mahusiano Wateja Wakubwa Bi. Shilla Senkoro katika maonesho hayo. photo6Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mwanga (kati) akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga. Photo7Mbunge wa Kilindi Mh. Beatrice Shelukindo akiwa na maofisa wa NMB alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...