Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 31, 2010

JATA chasaka dola 260 kusafirisha timu ya taifa

JATA chasaka dola 260 kusafirisha timu ya taifa

Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha Mchezo wa Judo (JATA), kinahitaji dola za kimarekani 260 ili kusafirisha wachezaji wao kushiriki mashindano ya Afrika, yanayotarajiwa kufanyika Juni 29 hadi Julai 3 mwaka huu, Afrika Kusini.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Kashinde Shaaban alisema, fedha mbali ya kuwa ni gharama za kuisafirishia timu lakini pia zitatumika kwa ajili ya mambo mengine yakiwemo maladhi na chakula.

Alisema hadi sasa hawana fedha kwa ajili ya kuanza maandalizi ya safari hiyo ambapo wanawaomba wadau mbalimbali wa michezo, Kampuni na watu binafsi kuwachangia kiasi hicho ili kuweza kuipeleka timu kushiriki mashindano hayo makubwa.

"Mashindano hayo ni makubwa hivyo kuyakosa haitakuwa vizuri kwani hiyo ni sehemu pekee ya kuweza kuonesha uwezo katika mchezo huo na kutoa nafasi kwa nchi zingine kuutambua na itasaidia hata kutafuta mapambano ya kirafiki hapo baadaye,'' alisema Shaaban.

Alisema wachezaji 12 na viongozi watatu wanatarajia kwenda nchini humo katika kushiriki mashindano ambapo kwasasa timu hiyo inaendelea na mazoezi katika Ukumbi wa Kisutu.

Alisema, wachezaji wengine wapo katika mazoezi jeshini na Kikosi Maalumu cha Ukonga ambapo wataungana na timu hiyo baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo ya hivi karibuni kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Alisema baada ya mashindano hayo timu itashiriki katika kambi mbili za nje katika vipindi viwili tofauti ambapo Septemba itakwenda nchini Cuba kwa ajili ya kuweka kambi ili kujiandaa na Mashindano ya Kitaifa yanayotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, Zanzibar.

NDOVU YATESA UGAIBUNI


Bw.Edwin Gafa, kiongozi wa Msafara wa Nile Breweries ya Uganda ambao wamepata tuzo ya kushiriki mara nyingi kwenye Monde Selection katikati ni meneja wa bia ya NDOVU Oscar Shelukindo

WAZANZIBAR WAPATANISHWA NA PRODUYUZA WAO




PAMOJA NA KUWA 2 BERRIES WAMEPATANA LAKINI WAENDELEA KUWA BERRY BLACK NA BERRY WHITE

Juzi nashukuru mungu nimeweza maliza tofauti kati ya berry white na berry black kwa kuwakutanisha tena katika uzinduzi wa album ya berry black (nafsi yako) na album ya chege (karibu kiumeni) bif ilidumu tokea mwaka 2006 walipotoa wimbo wa mwisho ulioitwa na wewe tu ft.shirko

Kwa sasa wapo peace lakini watabaki kila mmoja akifanya kazi kivyake na wanaweza shirikiana,so 2 berry haipo tena watabaki kutumia majina yao b white au b black
Walikuwa hawasalimiani kabisa na walikuwa kama chui na paka kwa sasa kama mnavyoona katika pics wapo peace kabisa
Nawashukuru sana na Amani idumu baina yao Inshallah
Kuendeleza Zenji Fleva

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUHAKIKISHA WANATENGA BAJETI YA MICHEZO MBALIMBALI


ABDALAH MAGONZA

Na Benedict Kaguo,Tanga

NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo,Joel Bendera ameziagiza Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha wanawatengea bajeti kwa ajili ya michezo,Maofisa Utamaduni ili waweze kufufua michezo kwenda sambamba na Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuhamasisha michezo hasa wa riadha.

Bendera alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa RCC kilichokutana kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa.

Alisema Halmashauri za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji hazina budi kutenga bajeti ili kuwawezesha Maofisa Utamaduni waweze kufanya kazi yao ya kuinua michezo mbalimbali katika Halmashauri hizo.

"Sote tunatambua kuwa michezo ni furaha,Amani,na ajira sasa ni vema Halmashauri zikatenga fedha kwa ajili ya maendeleo ya michezo kuanzia ngazi za chini"alisema Bendera.

Aliwataka viongozi wa Mkoa wa Tanga kushirikiana katika kuhamasaisha michezo ili kupunguza matatizo mbalimbali ndani ya jamii ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI,matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu.

WANACHAMBA SIMBA WAMTAKA ADEN RAGE


Na Benedict Kaguo,Tanga

WANACHAMA wa Klabu ya Simba Mkoani Tanga wamemtaka Mwenyekiti mpya wa Klabu hiyo,Ismail Aden Rage ametakiwa kufanya ziara za mara kwa mara Mkoani Tanga ili kuwamasisha wanachama kujiunga na klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao,Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoani hapa,Mbwana Msumari alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wanachama katika mkoa huo.

Msumari alisema wanachama wa klabu hiyo Mkoani hapa wanaimani kubwa na
Mwenyekiti huyo mpya wakiamini kuwa atasaidia kuiwezesha klabu hiyo
kujizolea sifa katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Hadi sasa klabu ya Simba Mkoani Tanga ina jumla ya wanachama hai,850
kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga.

Msumari aliongeza kuwa kwa sasa kuna jumla ya wanachama wapya 278 ambao
wameomba uachamana katika klabu hiyo ambapo ikiwa Mwenyekiti huyo mpya
atatembelea Mkoani hapa ataongeza chachu ya kuongeza idadi ya wanachama
wapya..

ZAIN YAKABIZI KOMPYUTA NA VITABU KATIKA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI


Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain, Muganyizi Mutta (kushoto) akimkabidhi makamu mkuu wa chuo kikuu Muhimbili 'MUHAS' Prof.Bakari Lembariti seti ya kompyuta pamoja na vitabu mbalimbali Dar es salaam jana vitu hivyo vimekabidhiwa baada ya kushiriki mashindano ya Africa Chalenge yatakayomalizika hivi karibuni kulia ni Mshauri wa wanafunzi Dkt. Ambrose Haule.(Picha na Rajabu Mhamila)
Meneja wa Mahusiano wa Kampuni ya Zain akionesha vitabu wakati wa hafla hiyo

mmoja wa maofisa wa chuo kikuu muhimbili akifatilia shuguli hizo leo

wanafunzi wakikabidhiwa vifaa na muganyizi muta wa zain

meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain, Muganyizi Mutta (kushoto) akimkabidhi makamu mkuu wa chuo kikuu Muhimbili 'MUHAS' Prof.Bakari Lembariti seti ya kompyuta pamoja na vitabu mbalimbali Dar es salaam jana vitu hivyo vimekabidhiwa baada ya kushiriki mashindano ya Africa Chalenge yatakayomalizika hivi karibuni kulia ni Mshauri wa wanafunzi Dkt. Ambrose Haule.(Picha na Rajabu Mhamila)

Wawnafunzi wa chuo kikuu cha muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain, Muganyizi Mutta (kushoto) akimkabidhi makamu mkuu wa chuo kikuu Muhimbili 'MUHAS' Prof.Bakari Lembariti seti ya kompyuta pamoja na vitabu mbalimbali Dar es salaam jana vitu hivyo vimekabidhiwa baada ya kushiriki mashindano ya Africa Chalenge yatakayomalizika hivi karibuni

WAIMBAJI MSONDO KUTOA ALBAM NJE YA BENDI HIYO


WAIMBAJI WA BENDI YA mSONDO NGOMA AMBAO WAPO MBIONI KUTOA ALBAMU YAO NJE YA BENDI HIYO WAKIIMBA WAKATI WA ONESHO LAO JANA KUSHOTO NI EDDO SANGA NA JUMA KATUNDU

Mwana mziki Juma katundu akiimba sambamba na wanenguaji wa bendi ya msondo ngoma wakati wa onesho lao lililofanyika katyika ukumbi wa Afri center Ilala Dar es salaa kushoto ni Amri Saidi super dongo na Nacho Mpendu Mama Nzawisa

TEA WAGAWA VIFAA VYA MAABARA SHULE YA UYOLE MBEYA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.Rosemary Lurabuka (kushoto) akifatilia mafunzo ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Uyole ya Mbeya walipokuwa maabara Mamlaka hiyo imetoa vitabu na vifaa vya mahabara hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita.(Picha na mpigapicha wetu)

BIA YA NDOVU YAPATA TUNZO


Oscar na Mzee Mkolwe wakiwa jumba la Kurhaus mjini Wiesbaden wikiendi hii ambako sherehe za Monde Selection za kutuza bidhaa bora duniani zinafanyika. Tuzo ya Dhahabu iliyopata kupitia bia ya Ndovu inatolewa leo katika ukumbi huo

Sunday, May 30, 2010

ZANTEL YAKABIDHI PIKIPIKI


DOMINICK KAVISHE TOKA MAGU AKIPOKEA ZAWADI YA PIKIPIKI TOKA KWA AFISA MAUZO MKOA WA MWANZA NZEKU CHIPA. ZANTEL INAENDESHA PROMOSHENI KABAMBE YA CHOMOKA NA PIKIPIKI KWA WAKAZI WA MWANZA NA MARA TU. ILI KUJIUNGA TUMA NENO PIKIPIK KWENDA 15583 NA UJISHINDIE ZAWADI KIBAO

FRANCIS MIYAYUSHO AMZIMA MKENYA ANTONY KARIUKI KATIKA RAUNDI YA 7


BONDIA FRANCIS MIYAYUSHO AKICHUANA NA ANTONY KARIUKI WA KENYA


MOHAMEDI CHIPOTA AKIMWELEKEZA JAMBO BONDIA YOHANA ROBART

MIPAMBANO ILIENDELEA HIVII

BONDIA FRANCIS MIYAYUSHO AKITAFUTA MBINU ZA KUMCHAKAZA BONDIA ANTONY KARIUKI KATIKA MPAMBANO WAO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA JANA

BINGWA WA MCHEZO WA KICK BOXER PENDO NJAU AKIFATILIA MPAMBANO UWO

ALLY BAKARI NA OMARI YAZIDU WAKIFATILIA KWA MAKINI MPAMBANO HUWO

MDAU SUFIANI MAFOTO AKIWA KATIKA HARAKATI YA KUCHUKUWA MAJINA YA WACHEZAJI

MAMBONDIA WAKONGWE WALIPOKUTANA KATIKA MPAMBANO HUO KUTOKA KUSHOTO NI SIMONI MLUNDWA RAJABU MLOWE RAJABU MHAMILASUPER D' EMANUEL MLUNDWA NA ANTONI LUTTA

MUSSA HASSANI AKICHUANA NA AUGWA MWITA KATIKA PAMBANO LA UTANGULIZI MUSA ALISHINDA KWA POINTI

MIYAYUSHO AKIPAMBANA KATIKA PAMBANO HILO

VIONGOZI WA TIMU YA NGUMI YA ASHANTI YA ILALA DAR ES SALAAM WAKIFATILIA MBAMBANO HUO JUMA MWALIMU NA EMANUEL MGAYA

MWANDISHI WA TANZANIA DAIMA LUHAZI LUHAZI AKIANGARIA NGUMI NA KONDO NASORO
Na Rajabu Mhamila

BONDIA FRANSCIS MIYAYUSHO ameendelea kutamba baada ya kumchakaza mpinzani wake Antony Kariuki katika pambano la kirafiki la kimataifa katika raundi ya saba mpambano uliofanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo Dar es salaam mwishoni mwa wiki katika pambano hilo raundi ya kwanza ilikuwa ya Francis kupiga ngumi ambazo zilionesha zaili kumuelemea Kailuki mali na hivyo aliokolewa na kengere raundi ya pili ilikuwa na mashambulizi kwa zamu ilipofika ya tatu Francis aliongeza kwa kutupa ngumi mbalimbali zilizomlevya Kairiuki na kuokolewa kwa kengere

Raundi zilizofuata mashambulizi yalikuwa huku na huku ambapo Kariuki arikuwa anacheza mchezo wa kujiami atimae ilipofika raundi ya saba ya mchezo huo Francis alingia kwa kupinga ngumi mfululizo na kuesabiwa baada ya hapo akaendelea kurusha makonde yaliyomsambalatisha mpinzani wake na kushindwa kuendelea na mpambano

Akizungumza baada ya mchezo huo Francis alisema mpinzani wangu amefanya mazoezi sana ndio mana amefika katika raundi hii lakini lengo langu lilikuwa kummaliza katika raundi ya kwanza ya pambano na akusita kumtaja kuwa anamuhitaji kwa hudi na uvumba asimu wake Mbwana Matumla

Mbali na pambano hilo kulikuwa na mapambano ya utanmgulizi yaliyowakutanisha kati ya Kijepa Omari aliyemshinda OMari Bomba kwa point nae Alfa George alimtwanga Yassin Ally kwa K.O ya raundi ya pili na mussa Hassan alimpiga kwa pointi Augwa Mwita nae Yohana Robert ailimshinda kwa point Issa Chalamanda na Ramadhani Kumbela alimshinda kwa K.O Ibrahim Hassan

Ambapo mapambano yote yalikuwa ya kirafiki

ZUNGA AITEKA ILALA KWA KUGAWA FULANA ZA JIMBO LAKE KAMA UTITIRI ILI WAJE KATIKA MKUTANO


MBUNGE WA ILALA AKINADI SERA ZA CHAMA CHAKE NA HALIYOYAFANYA KATIKA JIMBO HILO NA KUOMBA KUENDELEA KUWA MBUNGE

MEYA WA ILALA AKITETA JAMBO NA KADA WA CCM

MBUNGE AKIWA NA MMOJA WA MAKADA WA CHAMA CHEKE WAKATI WA MKUTANO WAKE


JOSEFU SENGA AKIPIGA PICHA MBUNGE
BAADHI YA WANANCHI WALIOHUDHURIA WAKISIKILIZA MADA MBALIMBALI

MWANDISHI JOSEFU SENGA WA TANZANIA DAIMA AKIWA KAZINI

mwandishi wa chanal teni faraja akizungumza na mbunge huyo

mbunge wa ilala mussa hazani zungu akihutubia katika mkutano huo

MBUNGE wa jimbo la Ilala Mussa Hazan 'Zungu' amefanya mkutano wa kutangaza hazma yake ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa ubunge jumapiri hii katika mkutano mkubwa uliofanyika mtaa wa tanga Ilala Dar es salaam ambapo kabla ya hapo wajumbe wa nyumba kumi kumi wa chama hicho kupewa fulana takilbani elfu kumi ili kuwagawia watu mbalimbali kwa ajili ya kufika katika mkutano huo uliotawaliwa na flana nyingi mpya za jimbo hilo

Akitangaza mambo mbali mbali aqliyoyafanya kipindi cha nyuma na kudai yeye sio msemaji wa leo bali anamuachia Mwenyekiti wa mkoa huo JOhn Guninita apate kuyanzungumza katika mkutano uwo na guninita alisema kuwa wameamua kumpa Zungu mamlaka tena ya kugombea Ubunge kwani wanaona nia yake ya kuleta maendele ya watu wanaozunguka katika jimbo hilo

Kwenye wengi pana mengi nikapata nafasi ya kuzungumza na mwana mama mmoja aliyekuwa katika mkutano huo akidai mimi mwana chama lakini jana wamepitisha fulana mimi awajanipa kwa kweli zungu ni mtu wa watu katika Wilaya ya Ilala anafika adi kwenye misiba nimeshughudia kwa macho yangu tuylipatwa na msiba jirani akaja akasaidi ila wapambe wake sio watu wazuri kwa kweli alisema mama huyo

Zungu kwa sasa amekuw akiwa kalibvu na watu mbalimbali kwa ajili ya kuakikisha anaendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia tiketi ya chama chake ya mapinduzi

CCM WAINGIA KULINDA MAJIMBO YAO


Waziri Mwakyusa na mbunge Kilasi kuhojiwa na Takukuru kwa kumwaga fedha majimboni mwao

Thobiass Mwanakatwe

Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya

SAKATA la Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof.David Mwakyusa na Mbunge wa Mbarali, Esterina Kilasi, wanaodaiwa kumwaga fedha na baiskeli katika majimbo yao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu sasa limetinga katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa Mbeya ambayo imeanza kuchunguza masuala hayo.


Pro.Mwakyusa ambaye ni Mbunge wa Rungwe Magharibi kati ya mwezi Marchi na April mwaka huu alitoa Sh.500,000 kila kata katika kata 19 za jimbo lake kwa madai zisaidie kuimarisha chama hali iliyozua mjadala mzito kutoka kwa wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Rungwe.


Awali fedha hizo alizikabidhi kwa viongozi wa chama wa kata husika wakati akiwa katika ziara jimboni mwake ambapo alitoa kwa kata 10 na baadaye kata nyingine 9 zilizokuwa zimesalia zilikabidhiwa kwa viongozi wa kata katika Ofisi za CCM za Wilaya kazi ambayo ilifanywa na Katibu wa CCM Wilaya ya Rungwe, Daudi Ilanga.


Kwaupande wake Mbunge wa Mbarali, Kilasi katika kipindi cha mwezi huo wa Marchi, anadaiwa kuwamwagia Makatibu wa Siasa na Uenezi wapatao 11 wa jimbo hilo Sh.100,000 kila mmoja ili wazitumie kama nauli ya kwenda Dodoma bungeni kutalii hali ambayo pia ilizua malalamiko kwa wananchi na wanachama wa wilaya hiyo.

Kilasi mbali na kutoa kiasi hicho cha fedha kwa Makatibu wa Siasa na Uenezi, pia aligawa baiskeli kwa Makatibu Kata 11 wa CCM wa jimbo lake ili ziwarahisishie kufanya kazi za chama kwenye kata zao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Wabunge hao wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti walithibisha kutoa fedha hizo kwa viongozi hao wa chama na kwamba walifanya hivyo kwa kuwa waliomba na pia walikuwa wanatekeleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya,Respick Ndowo, akizungumza katika mahojiano na Nipashe ofisini kwake jana, alisema taasisi yake baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari na wadau wengine wameanza kuchunguza madai ya wabunge hao wanaodaiwa kumwaga fedha majimboni mwao.

Ndowo alisema mbali na kuchunguza suala hilo, pia TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa madai ya wabunge wa mkoa wa Mbeya waliodai kuwa wapo watu wamemwaga mamilioni ya fedha kwenye majimbo yao kwa ajili ya kuwachafua ili wasiweze kuchaguliwa katika uchaguzi wa mwaka huu.

“TAKUKURU vilevile bado tunaendelea na uchunguzi wa madai yaliyotolewa na baadhi ya wabunge kwamba mafisadi wamemwaga fedha kwenye majimbo yao kwa ajili ya kuwahonga wananchi ili wawachukie na wasiwachague,”alisema Ndowo.

Akizungumza juzi wakati akihojiwa na kipindi cha Power Breakfast cha Radio Clouds FM, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk.Edward Hosea,alisema taasisi yake itawahoji wanasiasa waliotoa pikipiki,baiskeli na zawadi mbalimbali katika majimbo yao.

Dk.Hosea ambaye alikuwa akizungumzia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010,alisema,pamoja na uchunguzi kufanyika taasisi yake inaendelea kukusanya taarifa na itakuwa makini haitamwonea mtu wala kumsingizia na kusiistiza kuwa haitakurukupuka katika hilo

Alisema watu waliotoa vifaa hivyo vya usafirina vingine orodha yao ipo na wataitwa taratibu na kwa heshima kuhojiwa kujua vyanzo vya mapato yao na atakayeshindwa kujieleza atafikishwa mahakamani.

Mkurugenzi Mkuu huyo alisema inashangaza kuwa kwanini watu hao wapeleke zawadi hizo wakati huu unaokaribia uchaguzi na si wakati mwingine huko nyuma na kwamba wamekuwa wakipeleka vitu hivyo kwa watu mahsusi na si chama.

Alisema kama watu hao walikuwa na lengo la kusaidia vitu hivyo ilipaswa kutolewa mathalani kwa kijiji na isi kwa watu Fulani, hali ambayo inatia shaka kuwa vina lengo la kushinikiza watu hao wampigie kurwa mtu au chama fulani.

Kamanda huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya aliongeza kuwa kitu cha msingi kinachotakiwa kuzingatiwa na wabunge hao ni kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kama ni kweli wapo watu waliomwaga fedha majimbo watakapobainika hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja.

Alisema kama wabunge hao wanaona ni vigumu kwao kwenda ofisi za Takukuru zilizopo mkoani na wilayani waende hata kwa Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa au kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wakatoe maelezo ikiwezekana kutaja watu wanaowatuhumu kuhusika na ugawaji wa fedha hizo majimboni mwao.

“Tunawaomba wabunge kama wanaona ni vigumu kwenda kuja katika ofisi zetu za TAKUKURU basi waende hata kwa DC, RC au kwa RPC wakatoe maelezo, lakini hata hivyo hatutegemei mbunge ambaye ndiye anashiriki katika kutunga sheria akatae kuja kuja kutoa ushirikiano kwetu,”alisema Ndowo.

Katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu wabunge watatu walitoa maelezo kuwa wapo watu au mafisadi ambao wamemwaga fedha majimbo mwao ili kuwashawishi wananchi wasiweze kuwachagua.

Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la Lupa, Victor Mwambalaswa,Mbunge wa Mbeya Mjini,Bensoy Mpesya na Mbunge wa Kyela, Dk.Harrison Mwakyembe.

Saturday, May 29, 2010

ALLY CHOKI AFANYA MAKUBWA NA KUAIDI MASHABIKI KUENDEREA KUITUMIKIA EXTRA BONGO MPAKA MWISHO


Ali Choki aliingia na staili ya aina yake ndani ya ukumbi wa Msasani Club jana usiku tayari kwa utambulisho wa Bendi yake ya Extra Bongo. Baadae staili hiyo ilikuja kujulikana kama Igwee...! Choki haishi Vituko, Ni Burudni yaani kushangweka tu kila mtu kwa raha zake!
(Picha zote kwa hasani ya blogu ya www.mjengwa.blogspot.com )

ADRIANO ATIMKIA ROMA

Adriano atimkia Roma

Rome, Italia

MSHAMBULIAJI wa Flamengo, Adriano anajiandaa kurejea tena Italia. Mchezaji huyo wa zamani wa Internazionale amesema yuko mbioni kujiunga Roma.

Nina furaha kurejea Italia, nilihitaji kitu fulani kwa ajili ya kufuata wakati mbaya na ninahisi kuwa nimejitoa kwa watu wa Italia," alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Baada ya kujifunza sana nikiwa Flamengo, ninajijisi kuwa ninaweza kufanya vizuri. Ni uamuzi ambao nineufikiria kwa muda mrefu, kwani nimefurahi kwa kurejea makao makuu ya nchi.

Ni miongoni mwa sababu zilizofanya nichague Roma, Nimeona ni sehemu inayonifaa zaidi kuliko fedha. Ninapenda mipango yao wamekuwa wakinifuatialia mimi kwa miezi sita.

Ingawa uhamisho haujakamilishwa, Adriano anatumaini kuwa atavalia jezi za Giallorossi, ndani ya wiki chache.

Kwa asilimia 90 ni mchezaji wa Roma na nimezunguma na Rais wa Klabu, Rosella Sensi ili Juni 6, mwaka huu kumalizia usajili.

"Sina matatizo na Flamengo ya kuhamia niliondoka hapa kirafiki. Nilikuwa na furaha sana lakini leo (jana) ninajisikia muhimu kurejea Italia. Sitakia kurudia mambo yaliyotokea kwangu.

"Siko kwenye kiwango cha juu kama Francesco Totti, lakini ninasonga mbele kufikia kiwango chake na ninaweza kutoa mchango kwa Roma," alisema.

Inter yamng'ng'ania JOSE MOURINHO MPAKA KIELEWEKE


Inter yamng'ng'ania Mourinho

Rome, Italia

KLABU ya Internazionale, imesema haitakubali kumwachia kocha wake, Jose Mourinho kwenda Real Madrid bila ya kupambana.

Mabingwa hao wapya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamesisitiza kuwa hakukuwa na punguzo kwa kifungu kinachotaka kuvunjwa mkatana kwa euro milioni 16."

Real inadai kuwa Mourinho, atatambulishwa rasmi Jumanne lakini kuwamekuwa na mvutano katika klabu hizo mbili, Real haitaki kutumia kufungu cha kuvunja mkataba ikizingatia kuwa jambo hilo linamhusu Mourinho na Inter.

"Sifikiri kama inaweza kutatuliwa katika saa 24, lakini inawezekana tukamtambulisha Mourinho kwa vyombo vya habari wiki ijayo.

Ninaweza kusema Jumanne," Meneja mkuu wa Real, Jorge Valdano aliiambia Radio Nacional.

Wakala wa Mourinho alikutana kwa mara nyingine na Inter Alhamisi, lakini hakuna ufumbuzi ambao ulipatikana.

"Kifungu cha kuvunja mkataba ni euro milioni 16 na hakutakuwa na punguzo," alisema Mkurugenzi wa Nerazzurri, Marco Branca wakati akizungumza na Sky Sport Italia.

"Hatujashangaa kitendo cha Real kusema kuwa watamtambulisha Mourinho. Hatuna haraka na hii si siku ambayo itatatuliwa."

50 CENT AJIKONDESHA KWA AJIRI YA KUJINYIMA KULA


50 Cent ajinyima kula ili akonde

NEW York, Marekani

MWANAMUZIKI 50 Cent, amefanya mazoezi magumu ili kupungua uzito kwa ajili ya kuigiza filamu.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 34, mbali ya kufanya mazoezi amejinyima chakula kwa wiki tisa kwa ajili ya kucheza filamu, akiigiza kama mwanasoka wa Kimarekani anayepambana na kansa.

Nyota huyo wa In Da Club, alikuwa akitumia saa tatu kwa siku kwa kufanya mazoezi na kupungua uzito kwa ajili ya kucheza picha ya Things Fall Apart.

Mzaliwa huyo wa New York "Fiddy" ambaye jina lake ni Curtis Jackson, ametumia picha yake kwenye Twitter yake ambayo inaonesha jinsi alivyokonda kama mtu aliyeteseka kwa njaa.

Mbali ya kutunga nyimbo na kuimba, mwanamuziki huyo wa amekuwa na kipaji cha kuigiza filamu, amesema anawaza kama anaweza kurudisha mwili wake baada ya kuisha kwa filamu hiyo.

Vitali Klitschko kumvaa Sosnowski leo akishinda kupambana na David haye


Vitali Klitschko kumvaa Sosnowski leo

GELSENKIRCHEN, Ujerumani

BINGWA wa ngumi wa uzito wa juu Duniani wa WBC, Vitali Klitschko leo anatarajiwa kutetea ubingwa wake, dhidi ya Albert "The Dragon" Sosnowski.

Mzaliwa wa Ukraine, "Dr. Iron Fist" Klitschko, ambaye anaishi Hamburg, ataingia ulingoni katika uwanja wa Veltnis Arena mjini Gelsenkirchen akiwa na rekodi ya 41-2 (37 KO).

Sosnowski, ambaye ni mzaliwa wa Warsaw anayeishi Brentwood, England, ana rekodi ya 45-2-1 (27 KO).
Licha ya Sosnowski kuwa na rekodi nzuri katika miaka yake 12 ya kucheza ngumi za kulipwa, bingwa huyo wa zamani wa Ulaya haonekanani kama ni mahiri sana katika ngumi za uzito wa juu.

Sosnowski, ambaye ni mfupi zaidi akilinganishwa na Klitschko, ameachana na kupigania mkanda wa ubingwa wa Ulaya akitaka kuwania ubingwa wa Dunia.
Bado, Klitschko hamdharau mpinzani wake Sosnowski.
"Ninatarajia Albert Sosnowski atakuwa katika kiwango kizuri katika maisha yake," Klitschko alisema.
"Alisema atafanya kila kitu, ili kuweza kumchukua mkanda wangu, lakini nimejiandaa vizuri, lakini pia nimejiandaa vizuri na sitamdharau. Atakuwa na nguvu na kila wakati atakuwa akisonga mbele. Atafanya kila kitu kutaka kutwaa ubingwa."
Kocha wa Klitschko, Fritz Sdunek alitamba kuwa mteja wake yuko kwenye kiwango ambacho si cha kawaida na amejifuanza kupiga ngumu kali kwa ajili ya pambano hili.
"Kwa mara nyingine tena, amekuwa bora katika kupigana," Sdunek alisema. "Amefanya kazi sana kwa ajili ya miguu yake na alicheza zaidi ya raundi 110 za sparring,"
Klitschko alipoteza mechi mbili kutokana na kuumia ya kwanza ilikuwa dhidi ya Chris Byrd na nyingine dhidi ya Lennox Lewis. Klitschko hadi pambano linasimamishwa alikuwa akiongoza kwa pointi.

Sosnowski amerejea ulingoni baada ya kumtwanga, Danny Williams katika raundi ya tisa Novemba, 2008 na kisha alitoka sare na Francsesco Pianeta wa Italia katika mechi ya kuwania ubingwa wa.

Katika mechi yake ya mwisho, Sosnowski alitwaa ubingwa wa Ulaya kwa kushinda kwa pointi dhidi ya Paolo Vidoz wa Italia.

"Nimejiandaa vizuri na kuja hapa kutengeneza historia. Klitschko atanizuia mimi nafasi," Sosnowski alisema.

Sosnowski anatumaini kufanya vizuti katika mechi ya leo, ambayo inatarajiwa kutazamwa na mashabiki kiasi cha 40,000 mjini Gelsenkirchen.

Klitschko amekuwa na mtazamo wa kupigana na bingwa wa WBA, David Haye katika mechi yake ijayo, ambaye awali hakuweza kupigana na kaka yake bingwa wa IBF and WBO, Wladimir Klitschko.

MSHAMBURIAJI WA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA FERNANDO TORRES KUWA FITI WAKATI WA FAINAL ZA KOMBE LA DUNIA


Torres awapa matumaini Hispania

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Hispania, Fernando Torres atakuwa fiti wakati wa fainali za Kombe la Dunia, baada ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza na timu hiyo tangu afanyiwe upasuaji.

Juzi Torres alifanya mazoezi kwa muda wa dakika 45, sambamba na wachezaji wenzake 22, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana uwanjani, tangu afanyiwe upasuaji huo kwenye goti la mguu wake wa kulia Aprili 18, mwaka huu.

“Ni habari njema Fernando kujiunga nasi mazoezini. Kwetu sisi ni mchezaji muhimu na magoli yake ni muhimu sana,” alisema beki wa timu hiyo, Gerard Pique. “Natumaini atakuwa tayari kwa mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia,” aliongeza.

Hadi sasa mshambuliaji huyo wa Liverpool, tayari ameichezea timu hiyo ya taifa ya Hispania, mara 72 na kuifungia mabao 23 likiwemo bao lililoifanya timu hiyo, kutwaa ubingwa wa fainali za Mataifa ya Ulaya mwaka 2008, mbele ya Ujerumani.

Mbali na Torres mchezaji, Cesc Fabregas naye pia alifanya mazoezi na timu hiyo, huku kiungo huyo wa Arsenal akiendelea kupona mguu wake uliovunjika.

Katika fainali hizo, Hispania imepangwa kundi H ikiwa na timu za Uswizi, itakayokutana nayo Juni 16 kabla ya kuzikabili Honduras na Chile.

MASHABIKI A.KUSINI WABANIWA NA BRAZIL


Brazil yawabania mashabiki Afrika Kusini

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

TIMU ya taifa ya Brazil imewasili nchini Afrika Kusini, ikisema kuwa haitakuwa na urafiki na mashabiki na vyombo vya habari, kama ilivyofanya miaka minne iliyopita.

Habari kutoka nchini humo, zilieleza kuwa hatua hiyo ni kutokana na wachezaji na kocha kujaribu kuzuia kuzongwa na mashabiki, kitendo ambacho kinadaiwa kuliwafanya kutupwa nje ya michuano hiyo, hatua ya robo fainali nchini Ujerumani mwaka 2006.

Ilielezwa kuwa baada ya kuwasili nchini humo, timu hiyo ilikwenda kambini, ikiwa na matumaini kama walivyozoea mabingwa hao mara tano wa Dunia, lakini kwa haraka kocha Dunga akaweka wazi kuwa watajaribu kukaa mbali na mashabiki, ili kukwepa kuzingirwa na mashabiki.

“Kuanzia siku ya kwanza tulisema kipaumbele ni kwa timu ya taifa,” alisema Dunga. “Kitu kingine kitakuja baadaye kwani tunataka kufanya kazi ya timu ya taifa,” aliongeza Dunga

Naye Msemaji wa Shirikisho la Soka la Brazil, kupitia mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari nchini Afrika Kusini, alisema kilichojitokeza mwaka 2006 hakipaswi kutokea tena.

Mwaka 2006 timu hiyo ilikuwa ikifanya maandalizi yake kwenye ufukwe wa mji wa Weggis, Uswizi ambako wachezaji na kocha walisema hali ya hewa ingeifaa timu.

Wakati wa mazoezi hayo, mashabiki na waandishi wa habari walikuwa wakiruhusiwa kwenda kila mahali timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi na hatimaye, Brazil ikajikuta iking'olewa kwenye mashindano hatua ya robo fainali na Ufaransa, baada ya kuchapwa bao 1-0.

Hata hivyo mwaka huu vyombo vya habari pekee, ndivyo vitakuwa karibu na mazoezi ya timu, lakini si kwa mashabiki.

Kabla ya kuanza michuano hiyo, Brazil itacheza mechi mbili za kujipima ubavu dhidi ya Zimbabwe iyakayopigwa mjini Harare Juni 2 na mechi ya pili itakuwa dhidi ya Tanzania itakayofanyika Juni 7, mwaka huu.

Friday, May 28, 2010

WAREMBO MBEYA WADAI WAPEWE ELIMU FEDHA ZITAWEZA KUWAREVYA


wadai fedha zinawarevya mamiss,wataka wapewe elimmu kwanza

Na Moses Ng’wat,
Mbeya.

WAKATI mrembo atakayetwaa taji la miss Mbeya mwaka 2010 akitarajia kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja,wadau wa tasnia hiyo wametaka warembo wapewe elimu ya ujasiliamali ili waweze kuwekeza katika miradi,badala ya kutumia fedha hizo kutafuta umaarufu unaowadi na kujikuta kwenye mambo yanayowaletea kashfa.

Shindano hilo litaksalofanyika kesho mei 29 katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa
Jumla ya warembo 12 watapanda jukwaani kuwania umalikia huo wa mkoa,huku wakisindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya Dimond Musika ya jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa,Mratibu wa shindano hilo la mkoa wa Mbeya, Fanuel Ndonde,alisema washiriki hao 12 wamepatikana baada ya mchakato kufanyika katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Aliwataja warembo hao kuwa ni Jeinas Elias, Ntuli Coster,Ide Joghn, ZainabuMatagi,Laila Bashiru,Margareth Luca,Scola Haule,Zainab Shaban,Irene Gerald,Happness James,Shadia Mohammed na Grace Nashon.

Hata hivyo alisema kuwa tayari warembo hao wamlishaanza kambi tangu mei 24,chini ya walimu wao Sharifa Ally na Zaifa Ismail ambao walikuwa warembo wa mkoa kwa nyakati tofauti.

Alianisha kuwa zawadi kwa mshindi wa kwanza ni fedha tasilimu sh,milioni moja, mshindi wa pili shilingi 600,000, watatu shilingi 400,000, wa nne shilingi 300,000,watano shilingi 200,000 na warembo watakabaki watapatiwa kifuta jasho cha shilingi laki moja kila mmoja wao.
Aidha, alisema shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom,Tbl-kupitia Redds,Furniture Center Uhindini,ACL Ltd/ACESS Computer,UCC, Man Company ,PSI kupitia Salama Kondom,My Choice na Bomba fm.
Wadau hao walisema kuwa baadhi ya warembo wanaoshinda mataji na kupata zawadi ya fedha nyingi hujikuta wakishindwa kuwekeza katika miradi kwa ajili ya maisha yao ya baadae kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya ujasiliamali.
Walisema imefika wakati pia kwa waandaji na waratibu wa mashindano ya urembo kuanzia ngazi za mikoa kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya ujasiliamali ili kuwajengea uwezo warembo katika maisha ya kawaida baada ya kumaliza wa kutumikia mataji wanayoyapata.

Mmoja wa wadhamini hao ,Sadock Jonas ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Furniture Centre,alisema wameamua kutoa udhamini huo baada ya kubaini kuwa urembo ni taasisi ya kijamii hivyo inahitaji mchango ili iweze kuifikia jamii.

CBE NA UDSM WALIVYOTEMBELEA KIWANDA CHA BIA KUWAKILISHA MCHEZO WA POOL TABLE


WANAFUNZI WA CBE NA UDSM WALIVYOTEMBELEA KIWANDA CHA BIA NCHINI TANZANIA



kiwanda cha bia


wakiangalia jinsi chupa zinavyofunikwa na vizibo="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjncT3kpLKXi9H0mK643t52Id0qCNqdGac6tQjbqztKgxUaqgPK6kAHv6XlpH9h9_FVjlC3nsN9BTlM_JzG-M5-PerfaO7BtkOHY4reOMAcaZx8-V8MNBymkTb7c6QtTXFrYMfDxYDDsHNw/s1600/maabara.JPG">
wakipata maelekezo mbalimbali kuusu utengenezaji wa bia nchini

wakiangalia moja ya tanki la bia lililopo katki kiwanda hicho
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...