Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 9, 2010

FILAM YA KITANZANIA YA KIMATAIFA KUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI

Oscar Assenga,Tanga.

Filamu ya kitanzania yenye hadhi ya kimataifa inayojulikana kwa jina la( MAMBA WA ZIGI) hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuitoa kwa wananchi wa Tanzania na nje ya nchi.

Akizungumza mwandishi wa habari hizi aliyetaka kujua kuhusiana na maendeleo ya maandalizi filamu hiyo meneja msaidizi wa filamu hiyo Ramadhani Nyambuka alisema kuwa tayari watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi wamekuwa wakiulizia baada ya kuona matangazo kupitia mtandao maalumu wa filamu hiyo.

Alisema kuwa maandalizi mwisho yanafanyika kuweza kuitoa filamu hiyo inayolenga kuelimisha jamii kuhusiana na uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji kwa ujumla.
„Nimekuwa nikipokea simu nyingi hapa nchini na hata nje watu wakiulizia kuhusu lini filamu hii itakuwa tayari’’Alisema Nyambuka .

Filamu hiyo ya dakika 90 imeandaliwa kwa tekinolojia ya kisasa na inayokidhi viwango vya kimataifa ni aina ya filamu simulizi ambayo kwa kujibu wa Nyambuka itakuwa ni kipee hapa nchini.

Alisema filamu hiyo inayoandaliwa na mamlaka ya maji safi na maji taka Tanga Uwasa na kwa kusaidiwa kwa ukaribu na ofisi ya Rasi Tanga itaibua changamoto ya kimazingira inayoikabili bonde la mto zigi .

Alitaja changamoto ambazo zinakwaza ualisia wa mazingira hayo ni uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu katika chanzo cha mto zigi kilichopo amani wilayani Muheza pamoja na kukihtiri uvunaji miti katika msitu wa Longuza na biashara za mazao ya misitu(magogo).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...