Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 7, 2010

Osward Mweyunge mshindi wa Gofu Lugalo

Na Mwandishi wetu


Osward Mweyunge ameibuka mshindi katika mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kujipatia pointi 39.

Mashindano hayo ambayo yalishirikisha wachezaji wa rika mbalimbali yanadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.

Kufuatia ushindi huo Osward ambaye ni kati ya vijana wanaochipukia katika mchezo wa gofu, alizawadiwa Seti ya vyombo vya ndani kutoka kampuni ya Zain pamoja na zawadi nyingine.

Mbali na Mweyunge washindi wengine ni Juma Likuli aliyepata point 37, Terence Mwakaluka aliyejipati point 31, Joseph Taird aliyejipatia point 38, Mohamed Rweyemamu aliyejipatia pointi 34 na Simon Sayore aliyejipatia point 31.

Washindi hawa pia walizawadiwa zawadi mbalimbali kutoka Kampuni ya Zain ikiwemo muda wa maongezi wa mtandao wa Zain.
Mweyunge alitoa wito kwa wadhamini wengine kujitokeza ili kuhakikisha kuwa mchezo wa gofu unachezwa katika kiwango kinachokubalika kitaifa na hata kimataifa.
“Sasa tuna Zain ambao kwa kiasi kikubwa wanahamasisha watanzania kucheza gofu lakini kwa kutoa zawadi ambazo pia zinawatia moyo wachezaji, bado tunaomba wafadhili wengine kujitokeza kudhamini mchezo huu,” alisema.

Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania ina mkakati wa muda mrefu wa kuendeleza mchezo wa gofu hapa nchini kwa kushirikiana na klabu ya gofu ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam kuanzia kwa vijana wadogo ambao wana vipaji vya mchezo huo..

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...