Marquee
tangazo
Monday, October 31, 2011
FRANSIC MIYAYUSHO AMTWANGA MBWANA MATUMLA KWA POINT
Matukio Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel Kuelekia Fainali Za Mrembo Wa Dunia
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA JAJI WARIOBA
NBC na mabenki sita ya biashara yaingia makubaliano na (NHC)leo
Blogu Ya 8020 Fashion Yatimiza Miaka 5 Ya Utendaji Wake
Tukio hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa kusaidia wanawake MMWEI na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers kupitia kinywaji chake kikali cha Baileys
Saturday, October 29, 2011
AUNT EZEKIEL AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA PAMOJA NA WASANII WENZAKE LUKUKI
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili alisema ameamua kuiadhimisha kwa staili hii kwa kujumuika na badhi ya Watoto Yatima wa kituo cha Umri kilichopo Kawe Jijini Dar es Salam kwasababu yeye alitoka katika mazingira hayo mpaka kufikia hapo alipo, hivyo hujisikia furaha kujumuika na watoto yatima mahali popote anapokuwa haswa wakati wa furaha kama siku yake ya kuzaliwa, alisema Aunt Ezekiel.
Aunt Ezekiel katika sherehe hiyo alitimiza miaka 30 hivyo pia aliwahusisha wasanii wenzake mbalimbali kama JB,Dr.Cheni,Mboto,Wema,Cloud,Sinta,Chilele,na wengine wengi pamoja na marafiki zake ambao kila mmoja aliingia viwanja vya Leaders kwa staili yake haswa kwa kuonyesha umarufu wao kwa kumiliki gari la kifahari kila mmoja.
MBWANA MATUMLA NA FRANCIS MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO
wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha
Licha ya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali ususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.
Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.
Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D;
Twiga Bank ilivyoshiriki katika maonesho ya Wizara ya Fedha
Wake wa viongozi wa Jumuia ya Madola washiriki mkutano wa CHOGM 2011
Na Anna Nkinda – Perth, Australia
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni mmoja wa wake wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuia ya madola waliohudhuria mkutano wa siku tatu wa jumuia hiyo unaofanyika mjini Perth nchini Australia.
Wake hao wa viongozi walishiriki ufunguzi wa mkutano huo uliofunguliwa na Malkia Elizabeth wa pili na baada ya ufunguzi waliweza kuendelea na ratiba yao ya kujifunza na kujadili mambo mbalimbali yanayaikabili jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na afya, elimu, utamaduni, mila na michezo.
Baada ya kumalizika kwa ufunguzi huo walianza ratiba yao kwa kusikiliza mada kuhusu afya ya binadamu ilitolewa na Kanali Dk. Robert Walters ambaye ni Balozi wa Serikali wa afya ya binadamu na Julian Krieg Afisa mtendaji na mwalimu wa jamii katika mpango wa mkoa wa Afya ya binadamu.
Mme wa Waziri Mkuu wa Australia Tim Mathieson aliweza kuwatembeza wake hao wa viongozi maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makumbusho ya Australia’s Aboriginal and Torres Strait Islander ambako waliweza kujifunza historia ya nchi hiyo pamoja na utunzaji wa mila na utamaduni wao.
“Asili ya wenyeji wa nchi hii ni watu weusi ambao kwa sasa kizazi chao kinatishia kumalizika kutokana na uchache wao lakini miaka ya nyuma Waingereza walihamia hapa na kuzaliana na hivyo idadi yao kuwa kubwa kuliko wenyeji hivi sasa asilimia kubwa ya waustralia ni watu weupe.
Nchi hii inaongozwa na waziri mkuu Julia Gillard’s huku mtalawala wa nchi akiwa ni Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili”, alisema Mathieson.
Katika makumbusho hayo pia walijifunza mila za watu wa Magharibi ya Australia ambao wanaishi kandokando ya Bahari ya Hindi hivyo walifahamu utawala wao, faida wanazozipata hususani za kibiashara na utalii kutokana na matumizi ya bahari na bandari ambayo ni lango kuu la meli.
Waliweza kutembelea bahari ya Hindi na kujionea shughuli za biashara na utalii zinavyofanyika katika ukanda wa pwani, meli kubwa za mizigo zinavyotia nanga, kupakua na kupakia mizigo na kuona jinsi maaandalizi ya mashindano ya kimataifa ya mchezo wa mashua (Sailing World Championships) yanayotarajia kufanyika katika mji huo mwishoni mwa mwaka huu yanavyoendelea.
Thursday, October 27, 2011
VIPAJI MCHEZO WA NGUMI VINAINULIWA HIVI
Wednesday, October 26, 2011
FRANCIS MIYAYUSHO NA MBWANA MATUMLA WATAMBIANA MPAMBANO JUMAPILI
Mratibu wa mpambano wa ngumi Mohamedi Bawaziri katikati akiwa na mkanda wa ubingwa utakaogombaniwa na mabondia Fadhili Majia (kushoto) na Juma Fundi siku ya jumapili.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)