“SAFARI LAGER NYAMA CHOMA 2012” YATANGAZA BAA ZILIZOFANIKIWA KUINGIA FAINALI MBEYA.
Dar es Salaam, Jumatatu Feb 27, 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye hatua ya fainali mkoani mbeya baada ya mchujo wa awali kukamilika kwenye yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma 2012”
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Hotel ya Kebby”s Jijini Dar es Salaam Jaji mkuu wa mashindano hayo Bwana Douglas Sakibu alisema baa zilizochaguliwa kuingia hatua ya fainali jijini Mbeya ni.New Cit park,2000 Grocery,Makasini Bar,Savoy Bar na Free Park Bar. ambazo sasa zinasubiri siku ya fainali kwenye uwanja wa CCM Ilomba jumapili ya 04/03/2012
Alisema baa na majiko hayo yatakutana hapo mapema na kufanya shindano la wazi ili kuweza kumpata bingwa wa jiji hilo na wananchi watapata nafasi ya kujionea namna nyama choma inavyoandaliwa katika kiwango cha hali yajuu kabisa.
Baa hizi zilizoingia hatua ya fainali zote zina kiwango cha hali ya juu kabisa na hakika wameonyesha ujuzi na uzoefu mkubwa jambo linaloashiria kuwepo kwa ushindani mkubwa hivyo ni vyema wakazi wa jiji La Mbeya na vitongoji vyake wakawahi mapema jumapili pale Ccm Ilomba na kupata wasaa wa kushuhudia namna nyama zinavyoandaliwa kwa uhodari mkubwa huku wakiwa na bia yao waipendayo ya Safari Lager.
Kwa upande wake meneja wa bia ya Safari lager ambao ndio waandaaji wa Mashindano hayo Bwana Oscar Shelukindo aliwataka wakazi wa jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi siku ya fainali na pia mashabiki wa baa hizo kuja kuzishangilia na kuziunga mkono baa zao ili ziweze kuibuka washindi, sambamba na hayo bado kutakuwa na burudani nyingi toka kwenye bendi mbalimbali zitakazotumbuiza siku hiyo ili kuweza kutoa burudani kwa washabiki na wakazi wa jiji hilo kuanzia majira ya saa tano za asubuhi, pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washabiki zitakazotolewa.
Tutaendelea kuwa karibu na wapenzi wetu wa vinywaji toka Tbl hususani wa bia yetu ya Safari kwa kuwapatia burudani mbalimbali,Nyama choma bomba zaidi huku wakipata nafasi ya kujishindia zawadi kibao hivyo ni shindano ambalo mtu hapaswi kukosa hata kidogo.
Wakati huo huo majaji wa mashindano hay oleo wanafanya semina na baa zilizofanikiwa kuchaguliwa jijini Dar Es Salaam kasha kesho kuanza mchakato rasmi wa kuzitembelea kwenye maeneo yao kwa nyakati tofauti ili kuweza kupata baa zitakazofanikiwa kuingia hatua ya fainali hivi karibuni
Semina ya leo inazishirikisha baa za Huduma bar,Rosehill garden,Kilwa Road Pub,Pentagon Pub,Texedo Garden,Gadafi Square,Angels Pub,Fyatanga Bar,Jambo Lee,Hongera Bar,Braek Point Bar,Meeda Bar,Titanic Bar,Mangi Bar,Africenter Bar,Kisuma bar na Twiga bar .
.Alisema hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa na ubora wa hali ya juu.
Mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka jana washindi wa Jiji la Dar Es Salaam walikuwa Kisuma Bar ya Temeke Mwembe Yanga,Mbeya walikuwa Mbeya Canival,Kilimanjaro walikuwa Makanyaga bar ya Soweto na Arusha walikuwa SongaMbele Bar ya Sakina.