Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 14, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI ZANZIBAR.

Bi khadija Batash akitoa historia ya Marehemu Bakari Abeid Msanii Mashuhuri wa Zanzibar,katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 14/03/2012 huko katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar.
Wanafunzi kutoka katika Skuli ya Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakitoa burudani katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 14/03/2012 huko katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka skuli ya Vikokotoni Machano Bakari Hussen akipokea zawadi na Kumshukuru Mungu baada ya Kushinda katika chemsha Bongo ya Maswali ya papo kwa papo huko katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 14/03/2012 katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Abdalla Mwinyi akitoa hotuba katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 14/03/2012 huko katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar. Kushoto yake ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wa Zanzibar Bihindi Hamadi Khamis na kulia kwake ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA)Sudi Mohd Masoud.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...