Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 13, 2012

BENKI YA AKIBA COMMERCIAL KUBORESHA MAKAZI YA WATEJA WAKE KWA KUWAPATIA MIKOPO



HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA AKIBA COMMERCIAL BANK, BW. JOHN LWANDE, KATIKA UZINDUZI WA MIKOPO YA KUBORESHA MAKAZI, TAREHE 13 APRILI 2012, ACB BOARD ROOM.

Ndugu Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,

Habari za Asubuhi na karibuni sana ACB.

Ninayofuraha kubwa kuwakaribisheni kwenye hafla hii fupi hapa Akiba Commercial Bank. Hii ni benki ambayo inatoa huduma zote za kifedha kwa wananchi. Kwa hiyo uwepo wenu hapa naomba mjisikie kwamba mpo nyumbani, kwani ninyi vilevile hii ni benki yenu. Na kwa niaba ya uongozi wa Benki ya Akiba, ninashukuru sana kwa kuitikia wito huu.
Dhumuni hasa la kuwaalika hapa ACB leo hii ni kutaka kujumuika nanyi wanahabari katika uzinduzi rasmi wa aina hii ya Mkopo wa Kuboresha Makazi (yaani Home Improvement Loan). Leo ni siku kubwa kwa benki ya Akiba kwa vile tunazindua rasmi Mkopo huu wa Kuboresha Makazi, mkopo ambao ulikuwa ukiombwa na wateja wetu wengi. Kabla ya uzinduzi huu rasmi siku ya leo, kumekuwepo na matangazo mbalimbali juu ya huu mkopo kupitia radio na kwenye TV pamoja na billboards, mikakati yote hii ni katika harakati za kuwajulisha wananchi juu ya uwepo wa aina hii ya mikopo. Na katika kuweka msisitizo zaidi, nimewaalika hapa nikijua kwamba ninyi wanahabari ni kiungo kikuu kati ya taasisi na wananchi, hivyo mtatuwasilishia ujumbe huu kwa wananchi.
Katika harakati za kupanua uwigo wa huduma zinazotolewa na benki na kuimarisha huduma kwa mteja (Customer Service), ACB imeanzisha Mkopo wa Kuboresha Makazi ambao umetengenezwa kwa ajili ya wateja wa ngazi zote kuanzia mteja wa kawaida kabisa mwenye kipato cha chini, mteja wa kipato cha kati na mteja anayeinukia. Aina hii ya mkopo tunasema ni maalum kwa sababu inamwezesha mteja kuboresha makazi yake ama kumalizia ujenzi wa nyumba yake kama vile kuezeka kisasa paa ya nyumba yake, kupiga rangi nyumba, ama kufanya marekebisho ya kubadilisha vitu mbalimbali kama milango, madirisha kuwa ya kisasa, kupiga sakafu kwa ‘tiles, au kuongezea vyumba kama jiko, stoo, maliwato, fremu za biashara, nakadhalika. Na maboresho haya mteja huyafanya hatua kwa hatua kwa kadiri ya uwezo wake mpaka hapo atakapokamilisha jengo lake bila kupata msongo wa mawazo wa jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya maboresho hayo. Kiwango cha mkopo ni kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni ishirini. Kila mkopo utalazimika kurejeshwa kila mwezi, ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili yaani mwaka mmoja. Na mara tu mteja atakapomaliza kufanya marekebisho ya sehemu ya nyumba yake, anaruhusiwa kukopa tena na kuendelea hivyo mpaka atakapokamilisha.
Je ni mwombaji yupi mwenye sifa za kupata mkopo huu? Mteja awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea; Awe anamiliki biashara ambayo imekuwa hai kwa muda wa mwaka mmoja na kuendelea; Awe mmiliki halali wa makazi yanayoombewa mkopo na hapa atatakiwa awasilishe benki nyaraka zinazohakiki umiliki wake kama vile hati miliki, leseni ya makazi, hati ya mauziano, barua ya serikali za mitaa, hati ya kusafiria au kitambulisho halali.
Na kwa wale ambao tayari ni wateja wa ACB na wamewahi kupata aina zingine za mikopo kutoka benki hii au benki nyingine yoyote ile, na wanahitaji huduma hii ya Mkopo wa Kuboresha Makazi, waombaji wenye historia nzuri ya urejeshaji wa mikopo watapewa kipaumbele.
Kupitia kwenu wanahabari, napenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba huduma hii ya Mkopo kwa ajili ya Kuboresha Makazi inapatikana katika matawi yote ya ACB yaliyoko hapa Dar es Salaam ambapo tuna matawi yapatayo kumi na tatu katika maeneo mbali mbali ambayo ni Mbagala, Temeke, Buguruni, Tandale, Ubungo Plaza, Kinondoni, Kijitonyama, Tegeta, Kariakoo katika matawi ya Aggrey, Ilala (iliyoko ndani ya Machinga Complex) na Tawi la Kariakoo. Mikoani tupo Moshi mjini Mtaa wa Market na Arusha katika Jengo la Summit Centre. Aidha kwa wakazi wa jiji la Mwanza, tunapenda kuwajulisha kwamba ACB itafungua tawi lake jijini Mwanza hivi karibuni, na kwa wao pia wataweza kunufaika na huduma hii. Ningependa kuwakaribisha wananchi wote wenye kuhitaji huduma hii ya mkopo kwa ajili ya kuboresha makazi, wawasiliane na matawi yetu kwa maelezo zaidi ama kwa kuanza mchakato mzima wa kupewa huduma hii.
Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla kwamba benki yetu ya Akiba inazidi kuboresha huduma zake na kumrahisishia mteja aweze kupata huduma za kibenki popote atakapokuwa kupitia simu yake ya mkononi ambayo tutaiita ACB Mobile. Huduma hii itazinduliwa hivi karibuni na tutaitangaza rasmi pindi itakapozinduliwa. Kwa hiyo wateja wetu watarajie mambo mazuri zaidi kutoka Akiba Commercial Bank.
Kwa haya machache, napenda niwashukuru sana kwa kunisikiliza na ni matumaini yetu ACB kwamba mtayawakilisha haya kwa wananchi kwani azma na lengo la ACB si tu kuwaona wananchi wakiinukia kibiashara bali pia wawe na mahali pazuri pa kuishi na kuweza kuinua hali zao pamoja na familia zao kimaisha.
Ndugu wanahabari, naomba nitamke rasmi kuwa Mikopo kwa ajili ya Kuboresha Makazi (Home Improvement Loan) sasa imezinduliwa rasmi.
Asanteni sana.

4 comments:

  1. I was recommended this website by my cousin.
    I'm not sure whether this post is written by him as nobody else know such detailed about my trouble. You are incredible! Thanks!

    Also visit my blog; tvlinks

    ReplyDelete
  2. Hi, I do believe your website could possibly be having
    browser compatibility problems. When I look at your blog in
    Safari, it looks fine however, if opening in I.E., it's got some overlapping issues. I merely wanted to provide you with a quick heads up! Besides that, great blog!

    Have a look at my web blog; online tv
    My site - online tv

    ReplyDelete
  3. Normally I don't read post on blogs, but I would like to say that this write-up very pressured me to try and do it! Your writing style has been surprised me. Thanks, quite great article.

    my website ... rialaws.com

    ReplyDelete
  4. Very nice article, just what I wanted to find.


    Feel free to surf to my page :: www.closeyourhole.com

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...