Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 8, 2012

MAELFU WAOMBOLEZA KIFO CHA MWIGIZAJI WA FILAMU STEVEN KANUMBA


Meya wa jiji la Dar es salaam Bw. Didas Masaburi akizungumza na waandishi wa habari katika maombolezo ya msiba wa mwigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatcan jijini Dar es salaam, ambapo mamia ya waombolezaji wenye simanzi kubwa ,wamejitokeza katika msiba huo kwa wingi , hivyo kufanya jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na kufunga barabara inayokatisha eneo hilo kutoka Sinza kijiweni mpaka Tandale na Magomeni.


Katika picha kulia ni Kocha wa timu ya Coastal Union Jamhuri Kihwelo (Pereira) na katikati ni mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azan ambao nao wamehudhuria katika msiba huo.
Mmoja wa waombolezaji akijadili jambo na mwanamuziki wa bendi ya FM Academia Nyosh El Saadat na mwigizaji wa filamu Steven Jacob JB.
Kamati maalum ya mazishi ikiwa katika mkutano mkubwa wa maandalizi ya mazishi ya mwigizaji huyo kulia ni Eric Shigongo,Mussa Tagalile, Ruge na Ruge Mtahaba na wajumbe wengine.
Katibu wa Fedha na Uchumi NEC Chama cha Mapinduzi CCM Mwigulu Nchemba wa pili kutoka kulia, Mkurugenzi wa utamaduni wizara ya habari ,Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko na Katibu Mkuu wa Basata Gonche Materego ni miongoni mwa viongozi walihani msiba huo mkubwa katika sanaa ya uigizaji
Waombolezaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo leo.
Akina mama wamejitokeza kwa wingi katika msiba huo Steven Kanumba alikuwa ni kivutio cha watu wengi katika filamu zake kutokana na uwezo wake aliokuwa nao katika tasnia ya filamu nchini.

Waombolezaji wamejitokeza kwa wingi katika msiba huo kiasi kwamba hata sehemu ya kukaa imekuwa ni taabu, imebidhi kamati ya mazishi ikodishe ukumbi wa Vatcan Sinca kwa ajili ya wamombolezaji kpumzika humo.
Ulinzi umeimarishwa kabisa ili kuhakikisha hakutokei rabsha zozote katika msiba huo.
Hii ni Sehemu maalum iliyopambwa na picha ya marehemu Kanumba kwa ajili ya waombolezaji kusaini kitabu cha maombolezo.
http://www.fullshangweblog.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...