Marquee
tangazo
Friday, June 11, 2010
BENDI YA Manchester Music YAPANIA KULITEKA JIJI
wanamziki wa kundi hilo wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya waimbaji wa bendi hiyo
BENDI ya muziki wa Dansi ya Manchester Music ambayo ni changa inatarajia kutoa albamu yake ya kwanza itakayojulikana kwa ajina la 'Uridhi wa Baba' wanayotarajia kuizindua mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, msemaji wa bendi hiyo Abdalah Menssah alisema albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo sita ambapo kati ya hizo ni Urithi wa baba iliyobeba jina la albam, bomoabomoa, JK, Sina, Maneno si mkuki na Kijumbe wa mtaa.
Alisema bendi hiyo inaundwa na jumla ya wanamuziki 12 ambapo kati yao ni Saidi Ramadhani ambaye ametokea kundi la muziki wa asili la nchini Botswana 'Makhirikhiri', Sele Tamba aliyetokea TOT, Amina Remy, Bawili Salum na Saidi kosa aliyetokea makonde group.
Ramadhan amewataka wapenzi na wadau wa muziki wa dansi kusubiri kwa hamu ujio wa albamu hiyo na kwamba itakuwa na kila aina ya ladha wanazozipenda mashabiki wa muziki huo.
Alisema mbali na kuizindua albamu hiyo pia uzinduzi huo utakwenda sambamba na utambulisho wa bendi hiyo kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini na kwamba kwa sasa bado hawajajitokeza kwa watanzania ili kuwatambua.
kundi la bendi ya Manchesta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment