Baazi ya warembo watakaowania taji hilo
BAADA ya kuanza kambi juni 7,jijini hapa, warembo 12 bomba
kutoka mikoa ya Iringa,Mbeya, Rukwa na Ruvuma, kesho juni 21
, wanatarajia kuchuana vikali kuwania taji la Miss
nyanda za juu kusini kwa mwaka 2010,shughuli
itakayosindikizwa na msanii wa kizazi kipya Bell 9 kutoka
jijini Dar es salaam, katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa.
Wanyange hao wa mikoa ya nyanda za juu kusini,wanapanda
jukwaani wakiwa wamegubikwa na historia mbaya ya
kushindwa kutoa mnyange wa Taifa kama zilivyo kanda nyingine
za Mashari, Kaskazini,Kati na kanda ya ziwa.
Katika kinyanganyiro cha Vodacom miss Tanzania, warembo
waliowahi kuzipa kanda hizo umaarufu wakiiacha nyanda za juu
kusini kuwa chini ni Nasreem Karimu na Miriam Geraldwa kanda
ya Ziwa.
Lakini katika miaka 14, tokea mwaka 1994, Dar es
Salaam ambayo imegawanywa mara tatu katika kanda za Ilala,
Kinondoni na Temeke imetwaa taji hilo mara 12.
Ambapo katika kanda ya Kati,mwaka 1995, Emily Adolf
aliweza kuingarisha na kanda ya kaskazini katika mwaka
mwaka 1997 Saida Kessy, aliweza kuitoa kimasomaso kanda
hiyo.
Habari za uhakika kabisa zinadai kuwa kanda ya nyanda za
juu,iliwahi kufanikiwa kutoa mshiriki mmoja tu aliyefikia
katika hatua ya tano bora,ambaye ni Samia Mapondela.
Wakati kanda hii mwaka huu ikionekana kujipanga kuondoa
mkosi wa warembo wake kukosa nafasi za juu katika hatua ya
taifa,baadhi ya wadau wamekuwa na maoni tofauti,wengi
wakilaumu kwamba ushindi wa fainali hizo unaathiriwa na
historia kwa kuwa hata majaji nao wanaona mshindi hawezi
kutokea mkoani.
wachunguzi kadhaa wa masuala ya urembo wamekuwa wakiamini
huenda inatokana na kwamba waandaaji huamini kama mrembo
akitokea Dar es Salaam basi ni nafasi nzuri kwa wadhamini wa
mashindano hayo kujitangaza kwa wigo mpana japo waandaaji
hao kupitia mratibu wake, Hashim Lundenga wamekuwa
wakipingana na hilo.
Maswali yote hayo yanaweza yakajibiwa na idadi ya warembo
12 wa mikoa hii ya nyanda za juu kusini kwa kuwa wameonekana
kuwa bomba sana tofauti na miaka ya nyuma.
Mratibu wa shindano hilo nyanda za juu kusini Jimmy Tasha
kutoka kampuni ya Tasha Promosheni, akizungumza na waandishi
wa habari,alitamba kuwa mwaka huu ukanda huo utatikisa
katika fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
Aliwataja warembo hao kuwa ni Shadya Mohamed,Hapness
Jemes,Zainab Matagi na Iren Gerald wote kutoka mkoa wa
Mbeya.
Wengine ni Najath Makangira, Joyce Kangajaka na
Furaha(Ruvuma),Mary Kagali, Grace Simion na Rahma
Gege(Iringa), wakati Doreen Chambala na Agness Mgoma kutoka
mkoani Rukwa.
Tasha alisema zawadi kwa warembo watakaoshinda ni nono
ingawa hakuwa tayari kuzitaja,kwa kile alichodai kuwa bado
baadhi ya wadhamini wanaendelea na mchakato wa kuwasilisha
zawadi ambazo zitakuwa fedha taslimu na vifaa.
AIDHA, Tasha alisema kuwa shughuli hiyo itakayoanza majira
ya saa mbili za usiku katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa
,itafunguliwa na mgeni Rasmi ,mkuu wa wilaya ya Mbeya,Evance
Balama
Msimamizi wa kambi Zaifa Ismail ambaye licha ya kuwafunda
warembo hao pia alikuwa katika mstari wa mbele kuwaongoza
warembo katika kujifunza elimu ya ujasilia mali iliyotolewa
na baadhi ya wadhamini walipotembelea kampuni zao.
Akitoa maelezo kwa warembo hao pamoja na waandishi wa
habari, Msimamizi wa matukio wa kutoka kampuni ya bia nchini
(TBL), kupitia kinywaji cha Reds ambao ni moja wa wadhamini
alisema, jamii ya mikoa ya nyanda za juu inapaswa kujitoa
kwenye fikra potofu kuwa urembo ni uhuni.
Kwa upande wake meneja wa PSI, mkoa wa Mbeya Raphael Lyanga
alibainisha kuwa, kampuni hiyo haitaishia katika kudhamini
pekee bali katika msimu huu wambalozi wa kampuni katika kila
ngazi ya mkoa anayefamika kwa Miss Salama Kondom,ambapo
baada ya kumalizika mashindano ya ngazi ya mikoa wataendelea
kumtumia katika shughuli za kijamii.
Alisema lengo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa urembo si
fani ykihumni bali ni moja ya taasisi muhimu katika jamii
hususani katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto kubwa
ya magonjwa ndani ya jamii, hivyo warembo wanaweza kutoa
elimu ya magonjwa na uzazi wa mpango.
Shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom,Kampuni ya TBL,
kupitia Reds,PSI Tanzania,Mtenda Hotel Inn,Golden Folk
Hotel na Diploma
No comments:
Post a Comment