Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 8, 2010

Mabingwa wa Zain Africa Challenge 2010 CHUO KIKUU CHA EGERTO CHA KENYA CHANYAKUA DOLA 50,000 ZA ZAIN


Mabingwa wa Zain Africa Challenge 2010 kutoka Chuo Kikuu cha Egerton cha Kenya Baada ya kukabidhiwa kikombe cha ubingwa. Kutoka kulia ni George Ralak , Philip Chwanya, Mwalimu wao Emilia Ilieva,Ralph Obure na Ray Obiero. Mbali na kikombe mabingwa hao pia wamejinyakulia kitita cha dola 50,000 za kimarekani.
Na Mwandishi Wetu.
Chuo Kikuu cha Egerton cha Nchini Kenya kimeshinda mashindano ya mtoano ya Zain Africa Challenge, chemsha bongo ya mtoano ya kimataifa ya Vyuo Vikuu na kitaondoka na kombe la Zain pamoja na dola za Marekani 50,000, wakati kila mwanafunzi atapata dola 5000.

Chuo Kikuu cha Egerton kilipata pointi 740 na kukishinda Chuo Kikuu cha Africa Nazarene pia cha nchini Kenya ambacho kilipata pointi 510.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton walikabidhiwa Kombe la Zain na Mwenyekiti za Zain Uganda James Mulwana baada ya kuibuka na ushindi huo katika shindano lililorushwa kwenye luninga.

‘’Kwa niaba ya Zain nawapongeza kwa ushindi huu, hakika mmewasisimua watu wengi Barani Africa na kuifanya Afrika ijivune,’’ alisema Mulwana.

Wanafunzi kutoka Africa Nazarene kwa upande wao kila mmoja atandoka na dola za Marekani 2,500 wakati chuo chao kitapata dola za Marekani 25,000.

Zain iliwekeza zaidi ya dola za Marekani 1,000,000 katika mashindano ya ZAC mwaka huu. Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu Barani Afrika na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhawa kwa wateja wa Zain.

Chuo Kikuu cha Egerton kimeshinda mashindano ya ZAC mara tatu sasa na mara ya kwanza kilishinda kwa miaka miwili mfulilizo kabla ya kupokonywa ubingwa na Chuo Kikuu cha Ibadan cha Nigeria mwaka jana ambacho hata hivyo mwaka huu kilitolewa mapema katika mashindano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...