Marquee
tangazo
Saturday, September 4, 2010
MTIHANI WA DARASA LA SABA KUFANYIKA J3, J4 KAMPENI MARUFUKU KWA SIKU HIZO
MTIHANI wa Taifa wa kumaliza Elimu ya Msingi unafanyika kwa siku mbili za jumatatu na Jumanne katika shule zote za msingi nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantum Mahiza akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam alisema mtihani wa mwaka huu unatarajiwa kufanywa na wanafunzi 924,280 waliosajiliwa.
Alisema kati ya watahiniwa hao wasichana ni 471,827 na wavulana ni 452,453 ambao watafanya mtihani huo kwa lugha ya kishwahili na kiingereza.
"Kati ya wanafunzi 909,267 wakiwemo wasichana 464,523 na wavulana 444,744 watatahiniwa kwa lugha ya kishwahili na wanafunzi 15,013 wakiwemo wasichana 7,709 watatahiniwa kwa lugha ya kiingereza" alisema Bi. Mahiza.
Alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili wapo wanafunzi wa Elimu Maalum (walemavu),wenye uoni hafifu wanaotarajia kufanya mtihani ni 628 kati yao wavulana ni 246 na wasichana 382.
mtihani tayari imefikishwa katika kila shule na kwa mujibu wa taarifa za mikoa na Halmashauri, maandalizi yamekamilika na kuwataka wazazi kuwandaa wanafunzi hao kuhudhuria kufanya mtihani huo.
Bi. Mahiza alisema wizara yake inatarajia kuwa wanafunzi hao watafaulu kwa asilimi kubwa kutokana na matokeo ya kuridhisha ya mtihani wao wa majaribio (mork) waliofanya mwaka huu.
Alisema walimu, wazazi na viongozi washirikiane kuhakikisha wanafunzi wote waliosajiliwa wanahudhuria na kufanya mtihani wao kwa utulivu na kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Bi. Mahiza alisema watendaji watakaohusika katika usimamizi wanapaswa kufuata maelekezo mbalimbali waliyopewa wakati wa semina za maandalizi ya usimamizi mtihani.
"Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kinidhamu na za kisheria kwa yeyote atakayezembea au kuhusika na kasoro yoyote itakayoathiri ufikiwaji wa malengo yaliyokusudiwa" alisema Bi. Mahiza.
Alisema wizara yake inatoa wito kwa Makatibu Tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri na wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya maandalizi mapema ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha Kwanza mwaka 2011.Pia kampeni za uchaguzi zimepigwa marufuku kwa siku hizo mbili kutokana na wanafunzi kufanya mtiani wa Taifa
Naibu Waziri wa Wizara ya Elemu Bi. Mwantumu Mahiza akizungumza na waandishi wa habari kuusu kufanyika kwa mtiani wa darasa la saba Dar es salaam jana, siku ya tarehe sita,saba (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Bw. Zuberi Samataba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
majina ya walio faulu mtiani wa darasa la saba 2011
ReplyDelete