Marquee
tangazo
Wednesday, November 30, 2011
TIGO YAZINDUA SHINDANO LA ZAMU YAKO KUSHINDA
UBWA SALUMU AJIFUA KUMKABILI MUSTAFA DOTO DESEMBA 25
DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko
LONDON,
DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko kujadili uwezekano wa kufanyika pambano kati yao Machi mwakani.
Mpiganaji huyo wa London alitangaza kustaafu ngumi Oktoba mwaka huu lakini amesema kuwa yuko tayari kupigana tena kama atapata nafasi ya kurudiana baada ya kupoteza pambano lake Julai dhidi ya Wladimir Klitschko ambaye ni kaka wa Vitali.
Haye mchezo huo alisema: " Sijaona mkataba lakini kuna mazungumzo yanayoendelea.
"Nilisema kabla kabla ya kustaafu ningependa pambano hilo na kuna tarehe katika Machi ambayo imekuwa ikizungumziwa."
Mabondia hao wazaliwa wa Ukraine wamekuwa wakisema kwua mabalkuanalino yanafanyika ili kuwepo pambano la kuwania ubingwa wa WBC unaoshikiliwa na Vitali, baada ya Haye kupoteza pambano ambalo lilifanya apokwe ubingwa wa IBF/WBO dhidi ya Wladimir mjini Hamburg Julai mwaka huu.
Haye mwenyewe alisema amestaafu ngumi lakini yuko tayari kurejea ulingoni kama atajitokeza mmoja kati ya wanamasumbwi wa familia ya Klitschko.
Kumekuwa na mazungumzo kuwa huenda pambano hilo likafanyike Machi mwakani katika mji wa Dusseldorf Ujerumani.
JERRY MURO SASA YUPO HURU
Aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi. picha zaidi za tukio zitawajia hivi punde....stay tuned!
SERENGETI BREWERIES ANZISHENI VIWANDA NJE YA NCHI, PINDA
Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha kisasa cha Serengeti mjini Moshi leo (Jumanne Nov. 29, 2011) Mhe. Pinda alisema Kampuni hiyo lazima ijipanue kama vile wafanyabiashara wengine wa nje wanavyowekeza nchini.
“Kwa vile bidhaa yenu inapendwa hata soko la nje, anzisheni viwanda Burundi au Uganda… wenzetu wa nje wanafanya vivyo hivyo na kuwekeza hapa nchini,” alisema.
Kiwanda cha Serengeti Moshi, ambacho kimejengwa kwa ubia na Kampuni ya Bia ya East African Breweries Ltd. (EABL) ya Kenya ni cha tatu nchini. Vingine viwili vipo Dar es Salaam na Mwanza.
Bia ya Serengeti ilipata tuzo kwa kuwa ya kwanza katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Ireland hivi karibuni.
Waziri Mkuu pia alisema ataitisha kikao kitakachomjumuisha Waziri wa Kilimo na Chakula na wawakilishi wa Serengeti Breweries ili kuhakikisha namna bora ya kupata kwa uhakika mali ghafi muhimu ya kutengeneza bia, mtama.
Alisema mtama unaweza ukawa biashara nzuri kwa wakulima kwa kuwa Serengeti Breweries wanaununua kwa Sh. 600 kwa kilo moja ikilinganishwa na bei ya mahindi ambayo ni wastani wa Sh. 350 kwa kilo.
“Kuzalisha mtama ni gharama nafuu zaidi kuliko mahindi na kwamba zao hilo linastahamili ukame. Tukutane na Wairi wa Kilimo kuona namna ya kupata zao hili nchini kwa uhakika zaidi,” aliongeza.
Serengeti Breweries inahitaji tani 18,000 za mtama kwa mwaka, lakini upatijanaji wake hauna uhakika, Waziri Mkuu aliambiwa.
Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Manispaa ya Nairobi, Bw. Njeru Githae ambaye alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya; Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bibi Diane Corner na Mtendaji Mkuu wa EABL, Bw. Seni Adetu.
Mapema, kwenye Ikulu ndogo, mara baada ya kuwasili Moshi, Mhe. Pinda alisomewa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Leonidas Gama na kusifu jitihada za mkoa za kujietea maendeleo.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ATIA SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA
Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.
Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.
Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.
Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Novemba, 2011
NMB yazindua Kituo cha Biashara Arusha
BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha
WASHINGTON, Marekani
BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha uzito baada ya pambano lake dhidi ya Lamont Peterson litakalofanyika Washington mwezi ujao kama Timothy Bradley atakataa kupigana naye.
Kwa mujibu wa Dail Mail Khan, ambaye ni bingwa wa dunia uzito wa Light-welter atataka kutwangana na Bradley katika mechi ya kuunganisha mataji.
Bondia mwenye miaka 28, Bradley nsiye anaonekana anaweza kutoa upinzani mkubwa kwa Khan katika uzito wao, lakini amekuwa akionesha kuwa hataki kupigana naye.
Khan mwenye miaka 24, anaamini kuwa kama
Bradley ataendelea kugoma kupigana hatakwua na uamuzi mwingine ataacha na mapambano ya light-welter na mikanda yake na kuhamia katika uzani wa welter ili kupata mechi kubwa.
Kama pambano dhidi ya Bradley litakuwepo kwangu nitabaki katika uzito nilio nao lakini kama halitakuwepo nitahamia katika uzito wa welter,"alisema Khan.
Alisema anataka kupigana na mabondia wapya na na lihi ndilo linamsukuma kwa sasa.
"Tutaona kitu gani kitatokea baada ya mechi hii na kama pambano dhidi ya Bradley litafanyika. kama sivyo nitapandisha uzito."
Khan atapigana Desemba 10 kwenye ukumbi wa Convention Center, Marekani dhidi ya Peterson atakayekuwa nyumbani.
Khan alisema: "Nina mtindo ambao watu wanapenda, kasi na ngumi kali na kweli anamini kuwa ingawa Peterson atakwua nyumbani nitaaungwa mkono zaidi kuliko yeye siku hiyo.
"Hawajapata pambano la kusisimua Washington kwa muda mrefu kwa hiyo itakwua kitu kizuri kwao. Kila wakati nimekuwa nikitamani kupigana katika miji tofauti ili watu kupata nafasi ya kuniona mimi jukwaani.
"Nilitaka kupigana na Bradley na nikaja kupiugana na Marcos Maidana na Zab Judah na kuwapiga wote."
Monday, November 28, 2011
Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.
UTasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.
BAHATI NASIBU MPYA KUANZA DESEMBA MOSI
MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAENDELEO YA WANAWAKE ZANZIBAR (COWPZ)
RAIS DK JAKAYA KIKWETE MARA BAADA YA MKUTANO WAKE NA KAMATI YA CHADEMA JANA
Saturday, November 26, 2011
Haya tena Masudi aibuka na Upuuzi wake.Mambo ya Kutafuta Viji Senti tu
Mfumo nilioutumia ni kuongelea mambo mengi mchanganyiko na ili kuondoa uchovu wa kunitazama nikiongea, nimechanganya footages za videos, illustrations na animation (katuni) kuchagiza yale ninayokuwa nayazungumzia.
Ujumbe wa dvd hii ni nadharia ya vipande 26 vya keki. nikatengeneza MFANO wa uwepo wa idadi hiyo ya vipande vya keki ambavyo mara baada ya kuwekwa mbele ya watu (watanzania), kundi hilo la watu likataka kutoana roho ili kila mmmoja apate kipande cha keki hiyo, bahati nzuri wakatokea werevu (viongozi) ambao waling'amua kuwa kumbe idadi ya vipande vya keki (26) ni sawa kabisa na idadi ya watu waliokuwepo ambao walikuwa wanakaribia kutoana roho.
Werevu hawa wakawaambia watu hawa kuwa hatuna haja ya kung'oana meno wakati idadi yetu ni sawa kabisa na vipande vilivyopo, ukatengenezwa uataratibu wa kupanga foleni ili kila mmoja apite mbele achukue KIPANDE chake. baada ya kukubaliana hilo, bado werevu wakaona ni vema foleni hii iangalie walio dhaifu ili wawe mbele wawahi kupata keki kuchelea kuanguka kwa njaa.
Wakati vipande hivi vya keki vilipoanza kugawiwa, hawa viongozi, (watatu) wakaamua nao kwa kuwa ni sehem ya watu 26 kuchukua VIPANDE VYAO MAPEMA, bahati mbaya baadhi yao kutokana na kuwa karibu na meza ya keki na kutokana na ULAFI, wakaamua kuchukua zaidi ya kipande kimoja cha keki hali iliyopelekea watu wa mwishoni katika foleni ile kukosa vipande vyao.
dvd hii pia imeingia ndani kwa mafumbo kiasi kuangalia sababu inayopelekea watu kutaka kujipendelea zaidi kiasi cha kupelekea kudhulumu wengine, ikajaribu pia kuangalia dawa inayoweza kutumiwa kuepuka hali hii ya uchu na tamaa inayosababishwa na hofu ya kujiuliza nitapata lini na woga wa kuhofia kupoteza kidogo alicho nacho mkononi.
Kwanini umeitwa upuuzi? kwa sababu ya tabia na hulka za binaadam kupenda kupuuza kila kitu, ni hili nalo limetengenezwa ili ulitazame kisha ulipuuze.
Concept:
Ni documentary yenye sauti na picha za video pamoja na katuni mnato na katuni mtembeo (still cartoons and animation)
Wahusika wakuu: Masoud Kipanya
Itaingia lini sokoni: imeingia sokoni jana jumanne tarehe 15-11-2011 na inasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL.
Bei: Shilingi 3,000 tu.
Running time: Dakika 47
Sponsors: Hakuna mdhamini.Ila Blog ya Pr habari iko mbioni kuwa mdhamini wa kwanza
Future plans: Ni matayarisho ya upuuzi mwingine "WENYE NGUVU NA WAPAGAZI"
Nashukuru kwa ushirikiano wenu na mungu awabariki sana
MASOUD KIPANYA.
MKURUGENZI WA VODACOM TANZANIA AONGEA NA JUKWAA LA WAHARIRI
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza kushoto, kwa wahariri wakuu wa vyombo vya habari nchini Tanzania,wakati mkurugenzi huyo alipokwenda kujitambulisha kwenye mkutano wa Jukwaa la wahariri jijini Dares Salaam jana,katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano Mwamvita Makamba.