Afisa Masoko Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba amesema wajibu na jukumu la kuuwezesha Mlima Kilimanjaro kushinda ni letu, hivyo tuungane pamoja kama taifa na Vodacom inatoa fursa adhimu kwa watanzania kuuwezesha Mlima huo ambao ni fahari ya Tanzania kushinda na kuongeza sifa na kuendeleza heshima ya Tanzania katika ulimwengu.
Ili kushiriki mteja wa Vodacom anahitajika kutuma BURE ujumbe mfupi wa neno "KILI" au "KILIMANJARO" kwenda namba 15771 kuanzia leo hadi Ijumaa Novemba 17, 2011.
"Ni wakati wa kuonesha uzalendo wetu Vodacom inatoa fursa hii ya kipekee, kila mmoja aweke simu yake ya Vodacom wazi na apige kura, ni Imani yangu na ya Vodacom kwamba kwa nafasi hii isiyo na gharama Mlima Kilimanjaro utashinda tukitambua kwamba kila nchi inapigania kushinda moja ya nafasi saba zilizotangazwa."Amesema Mwamvita Vodacom inaungana na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watanzania kwa ujumla kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika kuupigia debe mlima Kilimanjaro kwa masilahi ya taifa.
"Kwa sasa Bonde la Ngorongoro linatuwakilisha katika orodha ya maajabu saba ya ulimwengu ambayo na hilo limetuletea sifa kubwa kama taifa, hivyo kwa kufanikiwa kuuongeza Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika kutaongeza sifa ya nchi mbele ya sura ya dunia sambamba na kukuza pato la taifa litokanalo na sekta ya utalii"Amesema Mwamvita Hatua ya Vodacom yenye wateja zaidi ya milioni kumi ya kutoa nafasi ya kwa wateja wake kushiriki kuupigia kura mlima Kilimanjaro bure ni hatua muhimu yenye kuendeleza sifa na mchango wa kampuni hiyo ya mawasiliano nchini katika masuala ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment