Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kupitia Chama cha Wananchi CUF, Hamad Rashid, akijumuika na vijana wa CCM pamoja na Msindai kucheza miondoko ya Taarab, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Wasanii wa kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakimpagawisha Mbunge Msindai, jukwaani wakati wakishambulia jukwaa.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Kapten John Komba, akiongoza kundi lake la Kwaya kuimba wimbo maalum wa Maadhimisho ya Sherehe hizo jukwaani.
Wasanii wa Kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakionyesha umahiri wao jukwaani wa kucheza Sarakasi.
Baadhi ya Wabunge na wananchi wakimtunza Kaptein John Komba wakati akiimba jukwaani.
HATIMAYE ULIFIKA MUDA WA KUANZA RASMI SHAMBRASHAMBRA ZA MAFATAKI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyesha Rimoti kufyatua Mafataki ikiwa ni sehemu ya kuzindua rasmi Mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kutoka (kushoto) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, baada ya kuzindua rasmi sherehe hizo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia
No comments:
Post a Comment