Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 23, 2011

AIRTEL YATOWA MSAADA KWA UVIMA


Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavisheakikabidhi moja kati ya Cherejani nne kwa Mwenyekiti chama cha UVIMA(toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kataya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaamikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidiana kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mke wa Raisi Mama Salama Kikwete.
UVIMA ni Umoja wa Vikundi vilivyo chiniya WAMA.

Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavishe akikabidhi moja kati ya Baiskeli nne kwa Mwenyekiti wa chama cha UVIMA (toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kata ya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidia na kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mke wa Raisi Mama Salama Kikwete.

Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi za UVIMA zilizopo Majohe
Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imewasaidia wakina mama wa kikundi cha UVIMA cha Mpiji Majohe kilichopo PUGU nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam kwa kuwapatia msaada wa Cherehani nne pamoja na Baiskeli nne ili zitumike kusaidia kuanzisha shule ya Ushonaji kwa manufaa ya kikundi hicho Wakizungumza katika hafla ya kupokea misaada ya baiskeli nne pamoja na vyerehani vinne kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Airtel wanawake wa kikundi cha UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMA kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa MPIJI MAJOHE uliopo PUGU DSM wamesema misaada ya namna hiyo imekuwa ikisaidia pia kukuza pato la Taifa. Leo hii misaada kama hii tunayoipata inasaidia sana sisi wakina mama wa UVIMA kuweza kuzalisha chakula na hatimae tutawasaidia watoto yatima waliopo mtaani kwetu na kwenye baadhi ya nyumba za wana kikundi, pia wajane pamoja na watu wenye uhitaji maalum alisema Bi Tatu Ngao Mwenyekiti wa UVIMA kata ya MAJOHE

Tunatoa ahadi kwa kampuni ya Airtel waje waone msaada waliotupatia leo baada ya miezi sita tutakuwa tumefanya mambo makubwa na mazuri zaidi aliendelea kusema Bi Tatu Ngao.

Kwa upande wake meneja huduma kwa jamii wa AIRTEL, Bi. Tunu Kavishe amesema AIRTEL itaendelea kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ujenzi wa Taifa. Airtel Tanzania Tulifahamu UVIMA kupitia WAMA na walitueleza jinsi UVIMA ilivyo na matarajio makubwa hivyo na sisi airtel tukaamua kutoa mchango wetu huu ili kuwezesha dhamira yenu yakusaidia wajane, watu wenye virusi vya ukimwi, wazee pamoja na Watoto yatima alisema Bi Tunu Kavishe Meneja Huduma kwa Jamii Airtel Airtel bado tunaendelea na mkakati wa kuhakikisha tunasaidia jamii kupitia sehemu zote muhimu ili kupunguza matatizo ya jamii ambayo pia nasisi tunaitegemea kuendelea kufanya Biashara yetu.

Mwakani tutaendelea kujitoa katika mambo muhimu ikiwemo Elimu pamoja na Afya ya jamii ili tuwe na wateja na jamii ya uhakika zaidi.alimaliza kusema Bi Tunu Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa ikitoa misaada ya aina mbalimbali katika jamii ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika huduma za jamii. Vikundi vya UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMA viko chini ya Uangaliazi wa Mama Kikwete na dhamira yake kuu ni kusaidia wakina mama, watoto yatima, jamii yenye virusi vya ukimwi, wajane pamoja na familia zenye uhitaji maalum kwa kuwapatia misaada na mbinu mbalimbali za kujikwamua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...