Bingwa wa ndondi za uzito wa juu duniani Wladimir Klitschko amefuta pambano la kutetea mataji yake dhidi ya bondia Mfaransa Jean-Marc Mormeck siku ya Jumamosi.
Klitschko, anayeshikilia mikanda ya IBF, IBO, WBO na WBA, alipelekwa hospitali siku ya Ijumaa kuondolewa jiwe katika figo yake.
Meneja wa Wladimir Bernd Bonte amesema: "Amesikitishwa sana na hatua hiyo lakini anajisikia maumivu sana."
Klitschko alimchapa bondia Muingereza David Haye kwa pointi mwezi wa Julai na kuweza kushinda taji la WBA.
Mormeck, mwenye umri wa miaka 39, ni bingwa wa zamani wa WBC na WBA uzito wa cruiser, aliwahi kuchapwa na Haye mwaka 2007.
Hata hivyo hajawahi kupoteza mchezo tangu alipoingia uzito wa juu mwaka 2009, akiwa ameshinda mapambano matatu dhidi ya Vinny Maddalone, Fres Oquendo na Timur Ibragimov.
Kaka yake Wladimir Vitali anashikilia taji moja tu la ubingwa duniani la uzito wa WBC ambapo alimshinda Tomasz Adamek kutoka Poland mwezi wa Septemba.
No comments:
Post a Comment