Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 30, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA LEO.


Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa. (Picha na Ikulu)
Rais Dk. Jakaya Kikwete pamona na baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka wakiongozwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Fennela Mukangara (wa kwanza kulia) katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...