Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 20, 2011

NDOVU SPECIAL MALT YAZINDUA KAMPENI YA ‘ANGALIA KWA UMAKINI’





Bw Gaudens Mkolwe, mpika bia wa Tanzania Breweries Limited (TBL) akiongea na waandishi kuhusu kampeni mpya ya Ndovu “Angalia kwa makini” leo jijini Dar es Salaam


Bw. Gaudens Mkolwe, akishika chupa yenye Crystal Malt ambayo ni kiungo ndani ya bia ya Ndovu.


Natalia Celani, Meneja Masoko wa Tanzania Breweries Limited (TBL) akiongea na waandishi baada ya uzinduzi wa kampeni mpya ya Ndovu jijini Dar es Salaam.


Meneja Bidhaa wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikuli akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Angalia kwa Makini”.

---

Ndovu Special Malt imezindua kampeni mpya ‘ANGALIA KWA MAKINI’ na kuwaalika wateja wake “kuangalia kwa makini” kile ambacho kinaipa Bia ya Ndovu ladha nzuri na ya kipekee, na kuifanya iwe bia bora zaidi yenye kiwango cha kimataifa.

Ndovu Special Malt imekuwa chaguo la wanywaji wengi wa bia nchini Tanzania ikiwa ni bia pekee ya kitanzania yenye hadhi ya kimataifa.

Ndovu ilithibitishwa kuwa na kiwango cha kimataifa pale iliposhinda tuzo ya juu ya Grand Gold katika tuzo za Monde Grand Selection mwaka 2010. Tuzo hizi za “Grand Gold” hutolewa kwa bia zenye viwango vya ubora unaoazia asilimia 90 mpaka 100. Mpaka sasa tuzo hii imetolewa kwa Bia ya Ndovu pekee.

Ni nini kinachofanya Ndovu iwe Bia ya kipekee?


Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli alisema “Ndovu ina kiungo cha kipekee ambacho wanywaji wachache wa Ndovu wanakifahamu. Ni kimea angavu, Crystal Malt ambavu ambacho hakipatikani ndani ya bia nyingine hapa nchini.

Kiungo hiki, crystal malt kimeandikwa kwenye nembo ya chupa ya Ndovu lakini watu wengi hawajaweza kutambua hilo. Kwa hiyo kwa kumsaidia mpenzi wa bia hii kufahamu kiungo hicho, kampeni mpya ya Ndovu ambayo tumeizindua hii leo inakusudia kumuwezesha mnywaji wa ndovu kutambua kiungo hiki kwa kutumia lenzi.

Gaudence Mkolwe, mpika bia mkuu wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) alisema “Crystal malt ni kiungo ambacho kiko ndani ya Ndovu na ndicho kinachoipa bia hii rangi yake ya dhahabu iliyokela na ladha laini ya kipekee. Hapa TBL tunajivunia sana kutengeza bia ya kiTanzania yenye ubora na tukiongelea ubora ni sawa na ubora wa kimataifa”

Natalia Celani, Meneja masoko wa Ndovu amesema “ Kampeni hii itatangazwa kwenye magazeti, mabango na kwenye baa mbalimbali hapa nchini. Pia kuna tangazo la redio linaloelezea jinsi kimea hiki kinavyoifanya bia ya ndovu kuwa ya kipekee, hivyo fuatilia kampeni hii na kama una lenzi tazama kwa umakini kwenye chupa ya Ndovu ili uone kiungo kinachoipa ladha ya kipekee bia hii”.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...