Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 8, 2012

BONDIA WA KIKE PENDO NJAO KUSTAAFU NGUMI NA KUWA MJASILIAMALI


Bondia Pendo Njau, akipozi na moja ya tuzo zake alizowahi kupata katika mchezo wa Kick Boxer.
*****************************
MWANADADA Mahiri katika mchezo wa Ngumi na Kick Boxer, Pendo Njau, amesema kuwa baada ya kujifungua salama wasalimini mtoto wake wa pili wa kiume hivi sasa ameanza mazoezi mepesi mepesi ya kujiweka fiti, wakati akijipanga kuachana na mchezo huo na kuwa mjasiliamali.

Tayari Pendo amekwisha anza maandalizi ya staili yake mpya ya maisha ya kuwa Mjasiliamali, ambapo kwa sasa anaweka mipango yake sawa huku akijiengua taratibu katika mchezo huo.

Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Pendo alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya maisha ya kila siku na kupanda kwa ugumu wa maisha, hivi sasa anajiandaa kusaka pambano moja baada ya kuwa fiti ambalo atatangaza rasmi kustaafu mchezo huo kutokana na kukosa maslahi na sapoti ya kutosha katika mchezo huo.

''We si unajua siku hazirudi nyuma bwana bali zinasonga mbele na familia ndo kama hivi, unadhani mwisho wa siku wanangu watarithi nini kama nimeweza kupigana siku zote hizo na kufanya vizuri lakini hadi leo hata Starlet au pikipiki tu sina ''. alisema Pendo

Aidha Pendo aliongeza kuwa kinachomfanya kutangaza kustaafu mchezo huo si kwamba ametokea kuuchukia bali ni kutokana na kukosa sapoti ya kutosha na wadhamini wenye nia ya kweli ya kuukuza na kuuendeleza mchezo huo.

''Mwaka juzi nilipata mwaliko wa mapambano matatu nchini Japan, lakini nilishindwa kwenda kutokana na kukosa msaada au udhamini wa kuniwezesha kusafiri ili kucheza mapambano hayo, na kutokana na kuwa nilishajiandaa kwa mazoezi ya kutosha kwa ajili ya mapambano hayo na kushindwa kusafiri, ikabidi niandaliwe mchezo wa kirafiki na Mwandada Rukia Nasirite kutoka Kenya, ambaye pia nilimchapa kwa pointi,

''Na pia hata mabondia wa uzito wangu wa Kg 60 (Light Weight) kwa hapa nchini bado ni wa kutafuta na hawajitokezi kutaka mapambano na mimi na ndiyo maana nikaona ni bora kwanza niwekeze katika familia yaani niongeze familia) kisha nirudi ulingoni kwa ajili ya kusaka pambano moja tu la kustaafu mchezo huu''.alisema Pendo

''Nimefikilia sana juu ya maisha yangu ya baadaye yanayotokana na kipaji changu cha mchezo huu na nikaona kuwa mwisho wa siku nitaishia kama walivyoishia mabondia wengine wakongwe na waliopata kutamba na kuwa maarufu ndani na nje ya nchi ambao hii leo nao pia hawana mbele wala nyuma zaidi ya kufaidi umaarufu wao wa siku hizo tu, ndiyo maana naamua
kustaafu mchezo huu''. alisema Pendo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...