*Mchezo wageuka Ulingo kama Misri, Wachezaji wamkimbiza mwamuzi kama Kuku uwanjani.
Pichani juu, ni kipa wa Yanga, Shaban Kado, akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
Katika mchezo huo Azam imeibuka na ushindi wa mabao 3-1, huku Yanga ikicheza pungufu wakiwa wachezaji 9 uwanjani baada ya wachezaji wawili, Haruna Niyonzima na Haroub Canavaro kupewa kadi katika kipindi cha kwanza cha mchezo kufuatia vurugu zilizotokea uwanjani hapo.
Mwamuzi wa mchezo huo, Israel Mongo, akitoka baruti 'Nduki' kuwakimbia wachezaji wa Yanga baada ya kutoa kadi mbili kwa wachezaji wa Yanga, jambo ambalo lilipingwa na wachezaji wa Yanga na kuzua mtafaruku uwanjani hapo.
Tukio jingine lililowashangaza mashabiki wa Soka waliokuwapo uwanjani hapo ni tukio hili la Askari Polisi aliyetinga magwanda, ambaye alitinga katikati ya uwanja wakati waa vurugu hizo na kuamulia ugomvi, jambo ambalo lingeweza kuamsha hasira zaidi za mashabiki.
Canavaro akitolewa nje baada ya kupewa kadi nyekundu.
Hamis Kiiza, akishangilia bao lake la kufutia machozi alilofunga katika kipindi cha kwanza baada ya kucheza One Two na beki wake, Shadrack Nsajigwa. Hadi mapumziko timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa ya bao 1-1 na mabao mawili ya azam ya ushindi yalifungwa katika kipindi cha pili, huku mchezo huo ukitawaliwa na kadi nyingi za njano.
Sehemu ya viti vilivyoharibiwa na kung'olewa uwanjani hapo vikiokotwa wakati wa vurugu zilizokuwa zikiendelea katikati ya uwanja.
Vijana wawili wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi, wakizaniwa kuharibu viti na kusababisha vurugu uwanjani hapo.
Waamuzi wa mchezo huo wakitolewa uwanjani hapo wakiwa chini ya usimamizi wa Polisi baada ya mchezo huo kumalizika.
No comments:
Post a Comment