Nahodha wa Timu ya TBC queens Bi. Grace Kingalame (kulia) akipokea zawadi ya mshindi wa pili kwa niaba ya timu yake shilingi milioni 2 na kombe kutoka kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya NSSF kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akizungumza na wadau wa michezo na washiriki wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kumalizika kwa fainali za mashindano ya 9 ya NSSF kwa vyombo vya habari na kutoa wito kwa taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini michezo mbalimbali nchini.
Kocha wa timu ya Habari ya Zanzbar Bw. Taibu Khamis akitoa somo kwa wachezaji wake mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo kati ya timu hiyo na timu ya NSSF jana jijini Dar es salaam.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Habari kutoka Zanzbar kikishangilia ushindi mara baada ya kutwaa kombe na fedha taslimu shilingi milioni 3.5 mara baada ya kuwaondoa wenyeji wa mashindano hayo timu ya NSSF kwa bao 4-0 leo jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa timu ya NSSF ya jijini Dar es salaam ambao ndio wenyeji wa mashindano ya 9 ya NSSF kwa vyombo vya habari akihaha kutafuta gori kutoka timu pinzani ya Habari ya Zanzbar wakati wa fainali za mashindano hayo jana jijini Dar es salaam. Timu ya Habari Zanzbar imeibuka kidedea kwa kuifunga NSSF bao 4- 0.
No comments:
Post a Comment