Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 1, 2012

BREAKING NYUZZZZZ........ANKAL AULA KWA KUANZISHA HUDUMA YA BURE YA WIFI


Rais Barak Obama wa Marekani akimtambulisha Ankal ambaye amechaguliwa kutunukiwa nishani ya kuwa mwana Libeneke Bora Duniani kutokana na mchango wake mkubwa wa kuunganisha watu mbalimbali duniani kwa njia ya mtandao huu wa jamii. Tuzo hiyo imetolewa na American Celebrities Guild na inaambatana na zawadi ya kitita cha dola 800,000 za Kimarekani. Hafla hii imefanyika leo huko Los Angeles.



Ankal amepewa heshima hiyo baada ya Globu ya Jamii kushinda tuzo ya Huduma Iliyotukuka hasa baada ya kuanzisha huduma za bure za mtandao, ambapo hivi sasa mdau unaweza kupata MichuziBlog Wifi bure katika kila sehemu iliyo na Hot Spot ya UhuruOne ambayo imeanzia jijini Dar es salaam wiki iliyopita na sasa juhudi za kuisambaza nchi nzima ili kuwafikia wadau wengi.



Ankal amealikwa kwenda Washington DC, Marekani kwenda kukabidhiwa tuzo hiyo na Rais Obama katika Ikulu ya Marekani Aprili 10 mwaka huu. pamoja na hio na zawadi ya kitita cha dola 800,000 za Kimarekani kama kifutia jasho na pia pesa ya kupanua wigo wa Globu ya Jamii.

Kwa habari zaidi ya huduma hiyo ya bure ya MichuziBlog Wifi


Mcheza sinema maarufu duniani Brad Pitt naye alikuwepo kuunga mkono tuzo aliyopewa Ankal ambapo yeye na mastaa wengi wengine walisaini mabango ya picha ya Ankal yatayosambazwa kila mahali duniani katika promosheni kabambe iliyoasisiwa na American Celebrities Guild na kutolewa kwa mtu anayejali maslahi ya jamii
Victoria Beckham, mke wa mwanasoka maarufu David Beckham, naye alikuwa miongioni mwa nyota kibao waliokuwepo kumsapoti Ankal na Globu ya Jamii. LIBENEKE OYE!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...