Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 10, 2012

NAIBU SPIKA JOB NDUGAI AFURAHISHWA NA TAMASHA LA PASAKA DODOMA

Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akipokea CD kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, inayoitwa "Utukufu Kwa Mungu"ya muziki wa injiili kutoka kwa Mwanamuziki Solomon Mukubwa wa DRC Congo, iliyozinduliwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe

Tamasha lingine kubwa limefanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Dodoma likishirikisha waimbaji lukuki kutoka hapa nchini na nje ya nchi kufuatia lile la jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo mwimbaji wa Afrika ya Kusini Rebecca Malope alitumuiza.
Mkuu wa Mkoa waa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza katika tamasha hilo leo jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto akiongea na wanadodoma kwenye tamasha hilo ambapo aliwahimiza wananchi wa Dodoma kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya amani nchini, Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Nduga na katikati ni Alex Msama.

picha na http://www.fullshangweblog.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...