Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 10, 2012

STEVEN KANUMBA KWELI ALIKUWA MTU WA WATU, MAELFU WAKO LEADERS KUMUAGA MCHANA HUU

Mwigizaji Clouds pamoja na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Mwigizaji mwenzao marehemu Steven Kanumba aliyefariki hivi karibuni kwa ajili ya kuuweka mahali palipoandaliwa kwa ajili ya waombolezaji kuuaga mwili wa mpedwa wao katika viwanja vya Leadres jijini dar es salaam, Marehemu Kanumba ataagwa leo hapo na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Fullshangweblog inarusha matukio haya kutoka mjini Dodoma kupitia sitelite zilizotegwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam
(PICHA NA MP)



Mwili wa marehemu Kanumba ukiwa umewekwa tayari kw awaombolezaji kuuaga kwa mara ya mwisho.
Waombolezaji wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Kanumba.
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa waombolezaji aliyepoteza fahamu kwa ajili ya majozi ya msiba huo.
Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wakiwa tayari kwa kuwahudumia watu watakaopata matatizo yoyote kutokana na msiba huo.
Mmoja wa waombolezaji akiwa anasaidiwa na mwenzake
Usalama umeimarishwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam kwa ajili ya msiba huo.
Kama unavyoona katika picha usalama ni mkubwa na watu wameandaliwa maeneo ya kukaa kwa ajili ya msiba huo.
Waombolezaji mbalimbali wakiingia katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Ni hali ya majonzi pamoja na kwamba kuna jua kali lakini waombolezaji wengi wamejitokeza katika viwanja hivi.
Makapeti mekundu yametandikwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupita viongozi na watu maarufu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...