Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 13, 2012

AIRTEL YAKABIDHI MILIONI 30 KWA MSHINDI WA NANI MKALI







Afisa uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha shilingi milioni moja kwa Camill Mayo baada ya kuibuka kuwa mshinidi wa siku na kujishindia shilling milioni moja katika promosheni Nani Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka kuwa washindi.


Afisa uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha shilingi milioni moja kwa Edward Mnewa baada ya kuibuka kuwa mshinidi wa siku na kujishindia shilling milioni moja katika promosheni Nani Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka kuwa washindi


Mshindi wa pili wa milioni thelathini wa promosheni ya Nani Mkali bwana Steven Chapile kutoka Arusha akikabidhiwa kitita hicho na Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa pili wa mwenzi wa promosheni ya Nani Mkali inayoendelea na kuwapa nafasi wateja wa Airtel kujishindia pesa taslimu.



Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya nani Mkali mara baada ya kukabithiwa pesa zao taslimu katika halfa fupi iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel leo, (wa kwanza kulia) ni Camil mayo akifatiwa na Edgar Mnewa waliojishindia milioni moja kila moja na (wa kwanza kushoto ) ni Steven Chapile aliyejishindia shilingi milioni 30.



Wateja wa Airtel kuendelea kujishindia mamilioni


Airtel yazawadia zaidi ya milioni 117 bado milioni 100 kushindaniwa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtanga na kumzawadia mshindi wa pili wa million 30 wa promoshenii ya Nani Mkali bwana Steven A Chapile ambaye ni nyabiashara na mkazi wa Arusha baada ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya mwenzi na kuzawadia kitita cha shilingi milioni 30 katika halfa fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Morocco leo.



Kwa mara nyingine Airtel kupitia promosheni ya Nani Mkali inaendelea kuzawadia wateja wake na kuwawezesha watanzania kujishindia mamilioni ya fedha taslimu, mpaka sasa zaidi ya shillingi milioni 117 zimeshazawadia kwa wateja wanaoshiriki na Kushinda na bado zaidi ya shilingi million 100 zipo kwaajili ya kuwazawadia wateja watakaoendelea kushiriki katika promosheni hii ya Nani Mkali.



Katika promosheni hii ya Airtel Nani Mkali washindi wa siku wanazawadia shilingi million 1, washindi wa wiki shilingi milioni 3 na wa mwenzi shilingi miliioni 30, mbali na kumtangaza mshindi wa shilingi Milioni 30, Airtel pia imewatangaza na kuwazawadia shilingi milioni moja kwa washindi 6 wa wiki ambao ni bwana Yunus Lugendo ambaye ni fundi umeme na mkazi wa babati, Jofrey Shangalawe mfanyakazi wa Tanesco na mkazi wa Shinyanga, David Samson Njole wa Mbeya, Denis Mugala ambaye ni mtumishi wa umma na mkazi wa Rukwa, Edgar Mnewa na Camil Mayo wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Dar es salaam.



Promosheni hii bado inaendelea kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...