Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 31, 2010

NGOMA AFRICA KUTUMBUIZA WORLD MUSIC FESTIVAL


Ngoma Africa wakitumbuiza katika mojawapo ya maonyesho yao.
Bendi maarufu ya watanzania yenye makao yake makuu nchini Ujerumani,Ngoma Africa, ni miongoni mwa bendi ambazo zinatarajiwa kutumbuiza hivi karibuni katika tamasha kubwa lijulikanalo kama World Music Festival zitakazofanyikia kando kidogo ya mji wa Kassel,Ujerumani,siku ya Ijumaa tarehe 23-25,Julai,2010.
Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya uongozi wa Ras Makunja,hivi karibuni waliimba wimbo wa kumsifu na kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete.Unaitwa Jakaya Kikwete 2010. Unaweza kuwasikiliza kupata habari zao kwa kutembelea www.myspace.com/thengomaafrica.

STARS KUKIPIGA NA MISRI NCHINI MISRI AUGASTI 11 HUKO KOCHA WA STARS KUWASILI LEO


TAIFA STARS.

Timu ya taifa ya wanaume taifa stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya misri Augasti 11 mwaka huu nchini misri ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za kombe la DUNIA nchini BRAZIL.

Msemaji wa TFF FLORIAN KAIJAGE amesema katika harakati za kutafuta timu wakafanikiwa kupata timu ya misri.

Mchezo huo unatambulika na FIFA kwani siku hiyo ya mchezo ni siku iliyopangwa na FIFA kwa ajili ya mechi za kirafiki za FIFA.

Wakati stars ikijiandaa na mchezo huo tayari kocha wa timu ya stars JAN PAULSEN anatarajia kuwasili jumamosi usiku kuja kukinoa kikosi cha stars

NA JANE JOHN

PHILOMON KYANDO DON KING WA TANZANIA KUMDHAMINI MMBWANA MATUMLA


DON KING

promota wa siku nyingi philomon kyando akiwa na rais wa zamani b.u.t Emanuel SAREHE

JUMA FUNDI AMTWANGA SHABANI KILUMBELUMBE K.O RAUNDI YA 9


JUMA FUNDI AKIPIGANA NA SHABANI KILUMBELUMBE KUWANIA UBINGWA WA DUNIA UNAOTAMBULIKA NA W.B.O

JUMA FUNDI KUSHOTO NA SHABANI WAKIPIGANA KATIKA MPAMBANO WAO ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM JANA

Friday, July 30, 2010

FAINAL MCHEZO WA POOL TEMEKE KUFANYIKA KESHO KILWA ROAD PUB


MCHEZAJI AKIJITARISHA KUPIGA MPIRA
WASHABIKI WAKIFATILIA MCHEZO WA POOL MASHINDANO YANAYODHAMINIWA NA SAFAR LAGER

TBS YATOA VYETI VYA UBORA



Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini Bw. Charles Ekelese akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Mariet Natural Bi. Marietha Putika
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini Bw. Charles Ekelese akimkabidhi cheti cha ubora Bi. Emalita Daudi wa Rukwa Food Processors
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini Bw. Charles Ekelese akizungumza kabla ya kugawa vyeti vya ubora vinavyotambulika na TBS nchini kulia ni Mkuu wa Idara ya Udhibiti Ubora Bi. Kazie Mwanga Mbwambo

BONDIA BADRU HASSAN ALIVYOUPENDA MCHEZO WA NGUMI



BADRU

BONDIA BADRU AKICHEZA KATIKA MOJA YA MECHI ZAKE

Na Shaban Mbegu

KAMA si mchezo wa masumbwi basi leo hii na mimi ningekuwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaowaniwa na klabu mbalimbali za soka kutokana na uwezo wangu wa kumiliki mpira nikiwa kama kiungo na wakati mwingine kucheza sehemu ya ushambuliaji.

Maneno hayo yamesemwa na Badrua Hassan 'Muhindi Mweusi' ambaye ni mmoja wa wanamasumbwi wanaounda klabu mpya ya mchezo ngumi ya Ashanti, ambayo imeonekana kufufua mchezo huo katika wilaya ya Ilala.

Akizungumza na gazeti hili Muhindi Mweusi anasema toka akiwa mdogo ndoto zake zilikuwa ni kuhakikisha anakuwa ni mchezaji tishio katika soka la Tanzania kama ilivyokuwa kwa wachezaji kama Abdallaha Kibadeni, Sunday Kayuni, Madaraka Selemani na Edibili Lunyamila ambao katika historia ya soka ya Tanzania na wao wamo.

"Nakumbuka katika miaka ya 90 niliwahi kusajiliwa na timu ya Oman FC ambako huko sikudumu sana kabla ya kujiunga na Matambo FC ambao nako pia sikuweza kukaa sana kabla ya kuhamia katika timu ya Six Villa nilipoweza kudumu kwa miaka kadhaa", anasema.

"Kutokana na kipaji nilichokuwa nacho nilijikuta nikihamahama kutokana na baadhi ya viongozi wa timu hizo kila walipokuwa wakinishuhudia mchezo wangu niliwavutia, na kutokana na umri wangu kuwa mdogo nilijikuta nikiwa nayumba katika maamuzi yangu na kusababisha kuwa situlii katika timu moja", anasema.

Anasema alijikuta anaachana rasmi na mchezo wa soka baada ya kuhama kutoka Bugurunin walipokuwa wakiishi na wazazi wake na kuhamia Ilala ambapo huko alikutana na vijana wenzake ambao walikuwa wakipenda zaidi mchezo wa masumbwi kuliko soka katika mtaa wao.

Anasema akiwa huko alijiunga na klabu ya mtaani kwao ambayo ilikuwa inaundwa na vijana mbalimbali waliokuwa wikiishi Ilala ambao walikuwa wakifanya mazoezi kila siku jioni na siku za mwishoni mwa wiki walikwenda katika fukwe mbalimbali.

Anasema baada kuanza kuonekana katika mapambano kadhaa ambayo walikuwa wakipanda katika ukumbi wa lango la jiji katika sikukuu mbalimbali kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili kutengeneza gym yao ya mazoezi, ambako huko alionekana na kuchuliwa na kocha George Kanuti ambaye kwa sasa ni marehemu.

"Kutokana na uwezo wangu wa kutupa makonde na kukwepa nilimvutia kocha Kanuti na kunichukua kunipeleka katika klabu yake ya Magomeni usalama ambako huko pia niliweza kung'aa kutokana na kushinda mapambano yote sita ya kirafiki niliyopigana kwa nyakati tofauti", anasema.

Anasema kutokana na uwezo wake aliokuwanao katika mchezo huo, kulitokea nafasi za kujinga na Jeshi la Wanachi Tanznia (JWTZ), ambao wao walikuwa wakihitaji mabondia kwa ajili ya kujiunga na jeshi lao.

"Nakumbuka wale viongozi wa jeshi walituona katika michezo ya kirafiki na kutukubali, tulikuwa kama watano hivi, lakini katika hali ya kushangaza mimi nilikataa kujiunga na jeshi na kuamua kukimbilia nchini Afrika Kusini kutafuta maisha", anasema.

Anasema ilipofika mwezi wa tatu mwaka 1999 aliamua kuzamia rasmi kwenda nchini Afrika Kusini kutafuta maisha ambako huko alidumu kwa miaka mitatu kabla ya mwaka 2003 kurudishwa nchini kutokana na kutokuwa na kibali halali cha kuishi nchini humo.

"Maisha ni mzunguko kaka, wakati nipo Ilala nikutana na wenzangu ambao walikuwa na mawazo ya kwenda mbele na kutokana na kuwa nao katika maisha ya kila siku nilijikuta na mimi nikitamani kwenda, nikafanya mpango na kuondoka zangu, ambapo huko pia nilikumbushia kucheza soka katika timu za mitaani na kukubalika", anasema.

Anasema baada ya kurudishwa nchini alijiunga tena katika klabu yake ya Magomeni pamoja na kuanzisha maisha mapya kwa kuanza kufanya biashara ya kuuza mitumba katika soko la Ilala, biashara ambayo anayifanya mpaka hivi sasa kutokana na kuitegemea kama ndio ajira inayoendesha maisha yake.

Anasema lakini mambo yalibadilika baada ya kocha wao George Kanuti kufariki, kitu kilichopelekea nyumba waliyokuwa wakitumia kama gym yao, kupangishwa kwa mtu mwingine na kusababisha kukosa sehenu ya kufanyia mazoezi na klabu hiyo kufa kabisa.

Bondia huyo anayepigana katika uzito wa kilo 55 anasema baada ya kifo cha kocha huyo waliamua kuanzisha ya kwao katika bustani ya maua iliyopo magomeni lakini kutokana na kutokuwa na vifaa walijikuta wakishindwa kudumu na klabu hiyo na kuamua kila mtu kufanya mazoezi kivyake.

"Kutokana na ubora wangu katika mchezo wa musumbwi kuna siku wakati nimemaliza pambano langu katika ukumbi wa DDC Kariakoo, nilikutana na kocha Rajabu Mhamira 'Super D' ambaye alionekana kunikubali na kunieleza nia yake ya kutaka niwe mmoja wa nitakaeunda klabu ya Ashanti", anasema.

Anasema kutokana na kutokuwa na klabu pamoja na kugundua kocha huyo anatokea katika wilaya ya Ilala alimua kukubali bila pingamizi na kujiunga rasmi na klabu hiyo yenye lengo la kufufua mchezo wa masumbwi katika wilaya hiyo.

Akizungumzia klabu yake mpya ya Ashanti anasema kwa kiasi kikukbwa kocha Super D ameweza kumbadilisha kwa kipindi kifupi ambacho wamekuwa pamoja na kuongeza kuwa katika kipindi hicho ameshapigana mapambano matatu ya kirafiki na kushinda yote.

"Naishukuru sana klabu ya Ashanti kwani imeweza kunifanya hivi sasa kujulikana katika medani ya masumbwi kutokana na kunitangaza pamoja na uwezo wa kocha wetu katika kutufundisha pamoja na kututafutia mapambano mbalimbali ya kirafiki ambayo yamezidi kutujenga", anasema.

Muhindi Mweusi pia alitoa shukrani kwa Shirikisho la ngimi za ridhaa nchini (BFT), kutokana na mchango wake kwa klabu hiyo ususani siku ya mapambano mbalimbali yaliyoandaliwa na klabu hiyo katika kuhamasisha mchezo huo ambapo kwa upande wa chama hicho kiliwakilishwa na Katibu Mkuu wake Makore Mashaga.

Bondia huyo pia aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia mchezo huo kama wanavyofanya katika michezo mingine, kwani bado mchezo huo unakabiliwa na changamoto nyingi kama vifaa vya kufanyia mazoezi.

"Tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutupa sapoti ili na sisi tuweze kuitangaza nchini yetu kupitia mchezo wa masumbwi ambao katika miaka ya nyuma ulipata mafanikio kutokana na mabondia kama Rashids Mtumla 'Snake Boy' na Joseph Malwa walivyoweza kuitanga nchi yetu", anasema.

Pia mchezaji huyo aliwataka vijana mbalimbali kuwa na malengo katika maisha ili waweze kupata mafanikio katika maisha yao, ambapo aliongeza kuwa kuliko kukaa vijiweni na kuvuta bangi basi wangekuwa na ratiba za kushiriki katika michezo mbalimbali ambayo katika miaka ya hivi karibuni imetokea kuwa ajira tosha.

"Katika maisha hakuna kitu kinachoshindikana kama kweli wana nia wateweza kupigana na wasiogope kujifunza mchezo huu wa ngumi kwa kuwa ni mchezo wa hatari kwani naamani kila mchezo una ubaya wake na uzuri wake cha msingi ni kuwa makini katika kitu unachokifanya", anasema.

Badru Hassani ambaye ni baba wa mtoto mmoja anayeitwa Yusra, ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya watoto tisa ya Mzee Hassani ambapo alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Karume, hakuendelea na kusoma kutokana na uwezo mdogo wa wazazi wake.

KUMEKUCHA VIJANA WA CCM KUPATA WAGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU


zamarad Mtetema akiomba kura kwa wajumbe
Zamaradi mtetema akisalimiana na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji
wagombea wakingia ukumbini

mmoja ya wawania ubunge kwa upande wa vijana akijinadi katika uchaguzi jana

TIMU YA SIMBA IKIWA MAZOEZINI KUJIANDAA KUKABILIANA NA YANGA KATIKA MCHEZO WA NGAO YA HISANI




MAZOEZI YANAENDELEA
WACHEZAJI WA SIMBA WAKIWA MAZOEZINI

Wilbrod Slaa AKIWA KATIKA MKUTANO


Mgombea wa urais wa Jamhuri wa Muungano kupitia Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, akiwahutubia maelefu ya wakazi wa mji wa Arusha, ambao walijitokeza kumdhamini, katika Uwanja wa NMC leo. Picha kwa hisani ya Joseph Senga

TIMU YA KRIKET YAENDA ITALIA


Mwenyekiti wa baraza la michezo taifa IDD KIPINGU akikabidhi bendera kwa timu ya taifa ya kriket ambayo imeondoka jana kwenda nchini ITALIA

Thursday, July 29, 2010

TBL ZAIDHAWADIA TASWA


Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milion 4.8 kwa Mwenyekiti wa TASWA FC,Majuto Omary kwa ajili ya mashindao ya Bonanza huko mkoani Arusha.katikati ni Afisa Uhusiano wa TBL,Lilian Erasmus


Meneja Uhusiano wa kampuni ya bia TBL Edith Mushi akizungumza na wanahabari katika ofisi za kiwanda hicho wakati alipokabidhi mfano wa hundi ya Shiilingi milioni 4 kama msaada kwa ajili ya Chama cha wandishi wa habari TASWA inayokewanda katika mashindano ya Bonanza yatakayofnyika mkoani Arusha jumapili.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetoa sh. 4, 875,000 kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA FC) kwa ajili ya kushiriki katika bonanza la waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TBL. Alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula na posho kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa siku zote watakazo kuwa Arusha. Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi alisema kuwa msaada huo ni moja ya kazi za TBL katika kusaidia jamii na safari hii wameamua kufanya hivyo kwa waandishi wa habari. Mushi alisema kuwa mbali ya msaada kwa jamii, lengo la TBL pia ni kudumisha ushirikiano wa karibu kwa waandishi wa habari ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya michezo na katika sekta nyingine hapa nchini. Alisema kuwa wanaamini kuwa mchango huo utaleta mafanikio kwa timu hiyo na kuweza kutetea vyema taji lake. “TBL inatambua na kuthamini mchango wenu katika maendeleo ya sekta mbali mbali ikiwa pamoja na michezo, tunayo furaha kubwa kuona leo hii mmekuwa mfano wa kuonyesha kwa vitendo mchezo wa soka, tunawatakia kila la kheri katika mashindano hayo na katika kazi ya kuelimisha na kukosa jamii,” alisema Mushi. Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary alishukuru TBL kwa msaada huo mkubwa ambao umeipa nafasi timu yake kutetea ubingwa wake ipasavyo. Majuto alisema kuwa TBL imeonyesha mfano wa kuigwa kwa jamii kwani imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia masuala mbali mbali ya jamii hapa nchini. “Hii ni faraja kuwa kwa TASWA FC kwa kuwa na kampuni yenye kujali waandishi kama TBL, tunaahidi kufanya vyema katika mashindano hayo na kuibuka na ushindi,” alisema Majuto. Alisema kuwa Tanzania kuna makampuni mengi sana, lakini kutokana na kutojua umuhimu wa waandishi wa habari, wameshindwa kuchangia punde waombwapo misaada, na mara nyingi wakitoa majibu ya barua ya maombi kwa njia ya simu siku tatu kabla ya safari ya kuwa ``ombi lenu halikufanikiwa’’. “Kwa kweli tumepata usumbufu mkubwa sana, kwani tulikuna vichwa ili kujua nini kifanyike ili kuikomboa timu na kufanikisha safari yetu,” alisema

MABONDIA KUONESHANA UMWAMBA DDC KARIAKOO KESHO


Bondia juma Fundi akipima uziti Dar es salaam leo kwa ajili ya mpambano wake wa kugombea ubingwa wa Dunia wa U.B.O kesho kushoto ni mpinzani wake Shabani Kilumbelumbe
Bondia Josephe Jorekera akipima uzito leo kwa ajiri ya pambano lake la kirafiki na Tomasi Mashari kesho katika umkumbi wa DDC Kariakoo kushoto ni mratibu wa pambamo hilo Aga Peter.

Wednesday, July 28, 2010

YANGA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA IJUMAA


SALUM MKEMI BABA YAKE NA SAMIA MRATIBU WA PAMBANO LA YANGA DHIDI YA TIMU YA TELECOM KUTOKA MALAWI.

Timu ya yanga itashuka dimbani jumapili wiki hii kucheza na telecom wander ya malawi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaofanyika uwanja wa uhuru jijini dsm.

Mratibu wa shindano hilo mkemi amesema maandalizi yamekamilika ila mpango ulikuwa timu hiyo icheze na simba ,yanga na azam lakini mpaka sasa ni yanga ambao wamekubali kucheza mchezo huo lakini bado wanendelea na mazungumzo na timu ya azam huku simba wakigoma kwa madai ratiba imebana

JESHI STARS YAIZIMA POLISI DSM KATIKA MICHUANO YA NETIBOLI YA KLABU BINGWA


Kama kawaida ya netiboli lazima uhangaike picha na jane john

Tuesday, July 27, 2010

SUMATRA YAKUTANA NA WADAU WA USAFIRISHAJI



Wadau wa usafilishaji wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini 'SUMATRA' uliofanyika DAr es salaam

MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA NETBOL YANAENDELEA TCC CHANG'OMBE DAR ES SALAAM


wachezaji wakiwania mipira wakati wa michuano hiyo jana

Monday, July 26, 2010

KIBAJAJI CHAMUOKOA MWENYEKITI



Mwenyekiti wa PR Habari akiseviwa na kibajaji katikati ya jiji

WADAU WANAMEREMETA




mchummmmmchumm mwaaaaaaaaaaaaaa
Said Omari Nang'ewa akiwa na mkewe Halima muogope baada ya kufunga ndo jana

MKOA WA ILALA WAMALIZA MASHINDANO YA MCHEZO WA POOL YANAYODHAMINIWA NA SAFARI LAGER


MSIMAMIZI WA MASHINDANO AKIOJIWA
Ofisa wa mauzo wa kampuni ya TBL Godrich Kalebi akiojowa na Jen John wa TBC
MAJAJI WA MASHINDANO WAKIPIGA HESABU
Mchezaji wa pool wa timu ya Kayumba ya buguruni, Festo Yohana akijitaarisha kupiga mpira wakati wa mashindando hayo katika ngazi ya mkoa yanayodhaminiwa na Safari Lager, yaliyofanyika katika ukumbi wa mashujaa vingunguti

WADAU WA NGOZI WAKUTANA LEO


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Bihashara DKT.Shaban Mwinjaka (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa ngozi iliyofanyika Dar es salaam

baadhi ya wadau wakifatilia semina hiyo leo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Bihashara DKT.Shaban Mwinjaka (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa ngozi iliyofanyika Dar es salaam
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...