Marquee
Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!
tangazo
Friday, January 21, 2011
SAFARI YA SIMBA BRAZIL YAOTA MBAWA
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Patrick Ochan, akijaribu kumtoka beki wa Atletico Paranaense ya Brazir, Endre Ernesto, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
Mabeki wa Simba Juma Jabu (kulia) na Haroon Shamte, wakishangilia bao lilillofungwa na Mussa Hassan mgosi kipindi cha kwanza baada ya Krosi nzuri iliyopigwa naye Juma Jabu.
Kiungo wa timu ya Simba, Jerry Santo (kushoto) akiruka kuwania mpira na beki wa Atletico Paranaense ya Brazir, Patrick Leonaldo, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Simba, Mbwana samatta (kulia) akimtoka beki wa Atletico Paranaense ya Brazir, Fransergio Rodrigues, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, akiwa na mchezaji wa timu hiyo, Uhuru Seleman, wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu hiyo na Atletico Paranaense ya Brazir kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Uhuru amerejea hivi karibuni kutoka nchini India alikokwenda kutibiwa.
"SAFARI YA SIMBA KWENDA BRAZIR HAIPO TENA"
Rais wa Kampuni ya RPB Oil, Rahma, akifanya mahojiano na Televisheni ya Channel 5, baada ya mchezo huo kumalizika. Rahma alisema kuwa safari ya Simba kuelekea nchi Brazir kwa ajili ya mchezo wa marudiano hautakuwapo kutokana na timu hiyo kushindwa kutimiza kama ambavyo alikuwa ameahidi kuwa iwapo ingewafunga wabrazir hao basi angeweza kuigharamia timu hiyo kuelekea Brazir kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment